MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI
HomeJamii

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komuniyo kutoka kwa Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oys...

FARAJA NYALANDU WINS WOMEN IN TECH AWARD IN SOUTH AFRICA
WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA
JK AWATUNUKU DIGRII WAHITIMU 1,179 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE






Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komuniyo kutoka kwa Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam leo. 
 
 
 
 
 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Pamoja naye (wa tatu kushoto) ni Dada yake, Ester Enock na anayefuata ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa. 
 
 
 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 
 
 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 
 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
 


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.

Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.

"Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.

"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.

"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI
MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtUvTWasD0thMm_10cY8ji9INhNnOVUu-bInlAp-1PAZxbp-eNSUYpcUkRr6bexlKNBx1FKnpuKjHhCyji0hB1ALSUizXxd_sSnYz73iNE-jIgzUHtcIbb0CGOcsasswzbRI4wrqFvkHM/s640/P+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtUvTWasD0thMm_10cY8ji9INhNnOVUu-bInlAp-1PAZxbp-eNSUYpcUkRr6bexlKNBx1FKnpuKjHhCyji0hB1ALSUizXxd_sSnYz73iNE-jIgzUHtcIbb0CGOcsasswzbRI4wrqFvkHM/s72-c/P+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mke-wa-rais-mama-janeth-magufuli.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mke-wa-rais-mama-janeth-magufuli.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy