WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA
HomeJamii

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe amekutana leo na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia H...

BALOZI WA CUBA NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe amekutana leo na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango na kuzungumza jinsi ya kusaidia utekelezaji wa mapendekezo 130 ambayo Serikali iliyakubali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu
 
Mhe. Waziri Mwakyembe amesema Serikali kama ambavyo ilivyoridhia mapendekezo hayo itasimama imara kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu na hivyo kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema nia ya Serikali ni kuona haki za bindamu nchini zinaheshimiwa bila ya kuingilia au kukiuka mila, tamaduni , desturi na imani za kidini ambazo Tanzania imekuwa ikizifuata au kuziamini tangu enzi.

Naye bw. Onyango alisema kwamba wao kama taasisi isiyo ya kiserikali wanafanya kazi na serikali mbalimbali duniani, taasisi zisizo za serikali na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinaimarishwa na kuthaminiwa na kuongeza kuwa lengo hasa la kukutana kwake ni kujitambulisha na kuomba kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha mapendekezo yaliyokubaliwa yanatekelezwa kikamailifu.

Pia aliomba kupatiwa nafasi ya kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji huo kwa taasisi na watumishi wa umma wanaohusika na utekelezaji wa mapendekezo hayo ili kufanikisha mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Alisema kwamba lengo lao kuu ni kuunganisha mpango wa tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini ili uendane na mpango wa malengo ya milenia ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli huku haki za binadamu zikiimarishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwezi Septemba 2016, Serikali iliyakataa mapendekezo 94, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130 kati ya 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar. Tamko hilo lilitolewa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR) mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa nchi wanachama uliofanyika mjini Geneva nchini 





Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.



Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA
WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ8vSCMxMfUPdo8Tqtw-KePL2cbDkWn55qr2JZuzvdRO2uKArBhR_ZZ6QuqCBXstYTnlYp0UajzqOWpqj7aQ-jkyU6pG6LnIZ_Xd-8unsSYwkXk5troyiOyUoEH30T09Z5T2JJoTtlNDw/s640/IMG_1497.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ8vSCMxMfUPdo8Tqtw-KePL2cbDkWn55qr2JZuzvdRO2uKArBhR_ZZ6QuqCBXstYTnlYp0UajzqOWpqj7aQ-jkyU6pG6LnIZ_Xd-8unsSYwkXk5troyiOyUoEH30T09Z5T2JJoTtlNDw/s72-c/IMG_1497.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mwakyembe-akutana-na-mwakilishi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mwakyembe-akutana-na-mwakilishi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy