NIDA YAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA KILIMANJARO
Mhe. Anna Mghirwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour na kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Rose Joseph.


HomeJamii

NIDA YAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA KILIMANJARO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa amezindua rasmi zoezi la Ugawaji Vitambulisho kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya ...

CHAMA CHA MAENDELEO YA MAKETE (MDA) WAPATA VIONGOZI WA KUDUMU
MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE
VIJANA KUJIANDIKISHA MASOMO YA TEHAMA YANAYOTOLEWA NA AIRTEL NA ATAMIZA YA DTBi


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa amezindua rasmi zoezi la Ugawaji Vitambulisho kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya Usajili wa Mkupuo kumalizika kwa asilimia 82%.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa zoezi la Usajili na Utambuzi liloanza mwezi Octoba 2017 kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi hilo; Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Rose Joseph amesema mkoa wa Kilimanjaro umekuwa mkoa wa nne (4) kitaifa kumaliza awamu ya kwanza ya Usajili Wananchi na kuanza kugawa Vitambulisho kwa wananchi waliokidhi sifa na vigezo vya uraia.

Amesema ugawaji wa awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa utafanyika kwenye ofisi za Watendaji wa Mitaa na Vijiji wananchi walikosajiliwa ambapo zaidi ya vitambulisho 250,000 vitagawanywa huku hatua za mapingamizi, uchakataji na uzalishaji wa Vitambulisho vingine zikiendelea kwa Wilaya zote za mkoa huo.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi; Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba amesema kukamilika Usajili wa Umma hakumaanishi wananchi hawataendelea kusajiliwa; badala yake kuwataka wananchi ambao hawajasajiliwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwenye ofisi za NIDA zilizoko kila Wilaya kwani manufaa ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni makubwa na mengi, na iwapo mwananchi atakosa kuwa na hati hiyo muhimu atakwama kufanikisha mambo mengi na muhimu ya kimaendeleo ikiwemo kushindwa kushiriki katika masuala muhimu ya kitaifa.

Mkuu wa Mkoa huo amewataka Wakuu wote wa Wilaya mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanahamasisha wananchi na kufuatilia kwa karibu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa kabla wananchi hawajaanza kukwama kufanya shughuli zao au kukumbwa na msako kwa kwa kukosa Hati hii muhimu inayowatambulisha kama Raia.

Sherehe za uzinduzi wa zoezi la ugawaji Vitambulisho mkoa wa Kilimanjaro zimehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Wafanya biashara, Viongozi wa kisiasa, wananchi, watu wenye mahitaji maalumu na vyombo vya habari; ambapo zaidi ya wananchi 20 wawakilishi wa makundi mbalimbali walikabidhiwa Vitambulisho vyao, huku wakuu wa Wilaya za mkoa huo wakikabidhiwa zaidi ya Vitambulisho 250,000 vya awamu ya kwanza.

Baadhi ya makundi wawakilishi wa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia kwa karibu matukio wakati wa sherehe za Uzunduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wanachi wa mkoa wa Kilimanjaro. Sherehe hizo zilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo.



Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza kwa ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bi. Rose Joseph na Kushoto ni Mhandisi Aisha Amour.



Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimkabidhi Ndg. Evance Moshi Kitambulisho chake kwa niaba ya kundi la watu wenye mahitaji maalumu.



Mwakilishi wa kundi la viongozi wa dini Sista Eliaichi Malisa akikabidhiwa Kitambulisho chake na mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wa sherehe za uzinduzi




Baadhi ya washiriki wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA -  Bi. Rose Joseph (kulia)




























Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NIDA YAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA KILIMANJARO
NIDA YAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA KILIMANJARO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivhBmliS8CJn0sqFQPTzMZQhUkK-cBUQtk2VbPgCfTe1vZaUnb-t18IZIOXp4bJym1VMh8tu-e7OEBYWYIWPjEPspX2cCVjloMVO-cpe5BkSKyjwZNOfkAPj5c7rXjPqLGMjcLEHXKHlE/s640/DSC_0462.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivhBmliS8CJn0sqFQPTzMZQhUkK-cBUQtk2VbPgCfTe1vZaUnb-t18IZIOXp4bJym1VMh8tu-e7OEBYWYIWPjEPspX2cCVjloMVO-cpe5BkSKyjwZNOfkAPj5c7rXjPqLGMjcLEHXKHlE/s72-c/DSC_0462.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/nida-yazindua-ugawaji-vitambulisho-vya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/nida-yazindua-ugawaji-vitambulisho-vya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy