Katibu Mkuu Award Mpandila akipiga kura wakati wa uchaguzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhcaguzi, Justino Jekela. Sehemu...
![]() |
Sehemu ya wajumbe MDA wakifanya zoezi la upigaji kura. |
![]() |
Makamu Mwenyekiti Philipo Mahenge (kulia) na Katibu Mkuu Award Mpandila wakipiga kura wakati wa uchaguzi huo. |
![]() |
Katibu Mkuu Award Mpandila akiwashukuru wajumbe kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa MDA, Clement Sanga na Makamu Naibu Katibu Mkuu, Monny Luvanda. |
![]() |
Baadhi ya wajumbe wakipiga kura |
![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Justino Jekela akiongea na wajumbe wakati wa shughuli ya uchaguzi huo. |
TAARIFA YA KAMATI YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA MDA ULIO FANYIKA AUGUST 27 2017*
Kipekee kabisa tunawapongeza Wanachama wote wa MDA na wasio Wanachama bali ni wapenda maendeleo ya Wilaya yetu ya Makete
Mnamo tar 09/07/2017 Kamati hii ndipo ilipokabidhiwa rasmi jukumu la kutunga *KANUNI* pamoja na *SIFA* za Wagombea kwa mujibu wa Katiba yetu ya MDA
Jumla ya wajumbe kumi na moja(11) tuliopendekezwa tulianza kuratibu shughuli nzima ya kuyafanyia kazi majukumu hayo pamoja na kwamba haikuwa kazi rahisi ila tulikubaliana na changamoto tutakazokutana nazo mbeleni
Hatimaye siku ya leo tumefikia tamati kwakuwapata Viongozi ambao tulikuwa tunawasubiria kwa hamu kubwa sana leo tumewapata, kwani wameshinda kwa asilimia mia moja kwa maana ya kura zote zilizopigwa zilikuwa ni za *NDIO* hivyo wafuatao wametangazwa rasmi kuwa Viongozi wetu wa MDA kwa muda elekezi Kikatiba
CLEMENT ANDREW SANGA
(MWENYEKITI)
PHILIPO HOSIANA MAHENGE (MAKAMU MWENYEKITI)
AWARD ASSA MPANDILAH
(KATIBU MKUU)
MONNY FARAJA LUVANDA
NAIBU KATIBU MKUU
Kamati inawapongeza sana wajumbe wote kwa ushirikiano wenu mzuri mlioutoa tangu kamati hii ianze kazi mpaka leo na tumejifunza mengi kupitia ninyi hivyo tuendelee kushikamana kama familia moja ya Makete
Pongez nyingi sana kwa Viongozi waliothubutu kuchukua fomu na kuzijaza na leo wamekuwa Viongozi ambao watatuunganisha Wanamakete wote kwa ajili ya Maendeleo ya Wilaya yetu
Mwisho kabisa tunawapongeza wote mliofika ukumbini na kuamua kwa moyo mmoja kupiga kura za NDIO kwa kila mgombea wa nafasi husika bila hata ya kura moja ya hapana hii yote ni ishara ya Ushindi kwa Viongozi wetu na Wanamakete wote kwa ujumla, sisi kama Kamati tumefarijika mno kwa kitendo hiki cha leo cha kiungwana na kiujasiri!!
Uchaguzi umeisha tuanze sasa Vitendo kwa spidi ya ajabu huku tukimtumainia Mungu peke yake na wala sio Wanadamu ambao mara zote hugeuka kulingana na mahitaji yao ya mwili kwa manufaa yao ya kibnafsi!!!
Asanteni sana Wanamakete wote!!
Wenu Katibu wa Kamati ya Uchaguzi -Hery Mbilinyi
COMMENTS