TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU
HomeJamii

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme...



 Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii



Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa
Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashina amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.

“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo
ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo
huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya
hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema
Dashina

Amesema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha
mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko kawaida.

Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.

Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo   kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika.


 Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA)  wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku 

 Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Leila Muhaji akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari juu ya kuimarika kwa Mfumo wa Ununuzi wa luku mara baada ya kuhamia sehemu nyingine. 

Waandishi wa habari habari walifika katika mkutano huo wakifatilia kwa Makini.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU
TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjlb3JPbjQquOetuOiaRTgU9rFOcPA2FPDAsUQHqE1qR0J4uJLCL3mlXRLVuTyvJj7CZ_gKv3cjG9-CH47Zj2zY_RESepf_kx8Wl-LxqlqATbUQPaGl0i9IP8gKnaHlSPQS0Ik44VnIDg8/s640/IMG_0046.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjlb3JPbjQquOetuOiaRTgU9rFOcPA2FPDAsUQHqE1qR0J4uJLCL3mlXRLVuTyvJj7CZ_gKv3cjG9-CH47Zj2zY_RESepf_kx8Wl-LxqlqATbUQPaGl0i9IP8gKnaHlSPQS0Ik44VnIDg8/s72-c/IMG_0046.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wake-juu-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wake-juu-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy