ASILIMIA 80 YA WANAOHITAJI DAMU NCHINI NI WANAWAKE.
HomeJamii

ASILIMIA 80 YA WANAOHITAJI DAMU NCHINI NI WANAWAKE.

Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wananchi hawapo pichani wakati ...

AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA
YUSUF MANJI AUNGANA NA FAMILIA YAKE, NI BAADA YA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KUFUTWA
UINGIZAJI WA MIFUGO KWENYE PORI LA AKIBA LA MKUNGUNERO UMEADHIRI UHIFADHI



Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wananchi hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam.


NA WAMJW-DAR ES SALAAM

ASILIMIA 80 ya wanaohitaji damu nchini ni wanawake kwa sababu mbalimbali ikiwemo uzazi salama wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida na njia ya upasuaji. 


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inafanywa na Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam. 


“Napenda kusisitiza Damu haiuzwi na kwa mgonjwa yeyote atakayeuziwa damu kwenye kituo chochote cha afya cha Serikali atoe taarifa kwenye idara husika na atachukuliwa hatua” alisisitiza Waziri Ummy Mwalimu. 


Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Uongozi wa Hospitali au kituo cha Afya cha Serikali wahakikishe kuwa wanaweka matangazo yanayoelimisha wananchi kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bila ya malipo na matangazo yaelekeze wananchi sehemu ya kutoa malalamiko. 


Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa wananchi hasa wanaume wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili kuweka akiba ya kutosha katika benki ya damu hatimae kupunguza uhaba wa damu katika benki ya damu na kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini Vanita Omary amesema lengo la kampeni hiyo ni kufikisha chupa 300 za damu katika uzinduzi hyo na tayari washapata chupa 288 mpaka sasa. 


“Tumeanza kampeni hii tangu jumatatu wiki hii na mpaka kufikia leo siku ya uzinduzi tumefanikiwa kupata chupa 288 tunatumaini tutavuka lengo mpaka mwisho wa kampeni hii, alisema Bi Vanita. 


Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo na Waziri Ummy imeandaliwa na Chama Cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini kwa kushikiana na Mpango wa damu salama nchini.
Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama kushoto akimsalimia mwananchi anayepata huduma katika moja ya banda lililokuwa likitoa huduma za afya katika viwanja vya Biafra wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.


Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa kike wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasnia ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasanii wakiwa wanasubiri huduma ya kuchangia damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ASILIMIA 80 YA WANAOHITAJI DAMU NCHINI NI WANAWAKE.
ASILIMIA 80 YA WANAOHITAJI DAMU NCHINI NI WANAWAKE.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_hOO7DkWg-BTWDwZgkiQrS_qh2Vggus5J1QrsFVk8tJROqGlD4mFPTfTCNgIx4kLhlei-yHqSvkmhr2WXjmFPnqwdbjB_kEsQRVkVqL-Hao6oudp7c0mF4MVepCgZFjFCacOyU1y0NgSt/s640/PIXi-5.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_hOO7DkWg-BTWDwZgkiQrS_qh2Vggus5J1QrsFVk8tJROqGlD4mFPTfTCNgIx4kLhlei-yHqSvkmhr2WXjmFPnqwdbjB_kEsQRVkVqL-Hao6oudp7c0mF4MVepCgZFjFCacOyU1y0NgSt/s72-c/PIXi-5.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/asilimia-80-ya-wanaohitaji-damu-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/asilimia-80-ya-wanaohitaji-damu-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy