AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA
HomeJamii

AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) baada ya kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea...

SERIKALI YAAHIDI KUANGALIA UPYA MAFAO YA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA
MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
TANZIA: MAREHEMU FELIX KAPINGA ATAZIKWA LEO TAREHE 06/12/2016 MKOANI NJOMBE





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) baada ya kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017. Kushoto ni Balozi wa Ireland Nchini, Mhe. Paul Sherlock.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ireland Nchini, Mhe. Paul Sherlock (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. David Omozuafoh (kulia) baada ya kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.


Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.Kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.

NA OWM, DODOMA
WAZIRI Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa amesema Mataifa ya Afrika yanatakiwa yaandae maarifa, vitendea kazi na rasilimali watu watakaoweza kusimamia na kuendeleza ipasavyo sekta ya madini na kuleta tija kwa Taifa husika na wananchi kwa ujumla.


Amesema taarifa za kijiolojia zinaonesha kuwa Afrika ni Bara lenye utajiri mkubwa wa rasilimali madini huku sehemu kubwa ya madini hayo yakiwa bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji.


Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 14, 2017) alipofungua mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo hicho mkoani Dar es Salaam.


Waziri Mkuu amesema rasilimali za madini ilizopo Barani Afrika inaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi nyingi iwapo itasimamiwa vizuri.


Ametolea mfano Tanzania ambayo licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, almasi, chuma, madini ya vito kama tanzanite lakini mchango wa sekta ya madini ni asilimia 4.8 ya pato ghafi la Taifa.


“Changamoto kuu kwa sasa ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa na sekta ya madini inayotoa mchango stahiki katika nchi husika pamoja na kusimamia sekta hii kwa kuwafanya wananchi wetu hususan katika maeneo yenye rasilimali wakanufaika na kuona fahari badala ya kuacha mashimo, umasikini na mateso kwa wananchi.”


Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ambacho leo kimetimiza miaka 40 ni kuhakikisha sekta ya madini inawajibika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi pia ikijali masuala ya mazingira, hivyo ni vema kikatumika kama ilivyokusudiwa.


Waziri Mkuu amesema kituo hicho kikitumika vema kwa mujibu wa kusudia la uanzishwaji wake kinaweza kuleta tija kubwa kwenye sekta ya uchumbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta.


Amesema kituo hicho ni moja kati ya taasisi chache duniani yenye teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kusaidia kufanya uchambuzi wa miamba na madini yaliyimo. “Pia ni sehemu ambayo unaweza kupata huduma za ushauri na kusaidia teknolojia utakayoweza kutumia ili kufanya uzalishaji wa madini mbalimbali.”


Hivyo amewakumbusha wajumbe na wanachama wa AMGC kuwa kituo hicho hawajakitumia ipasavyo ni vema kikatumika ili kupata tija kwenye uendelezaji na usimamizi wa madini, ambapo ameiagiza Bodi iandae mpango utakaoziwezesha nchi wasnachama kukitumia.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ya kwanza ni kwa wanachama kutolipa ada kwa wakati.


Dkt. Kalemani ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha AMGC amesema changamoto ya pili ni wanachama wa kituo hicho kutokitafutia wateja na masoko. Pia miundombinu mingi ya kutuo ni chakavu.


Akizungumzia changamoto hizo Waziri Mkuu ameziagiza nchi zote zinazodaiwa ada ikiwemo Tanzania zilipe ada stahiki kwa wakati na kuweka mkakati wa kukitangaza kituo hicho ili kukiwezesha kupata wateja kwa ajili ya kutumia huduma zitolewazo.


Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitoa maelezo kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwake ) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA
AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOq9Du0zNanf7UC6yuTZZ1vpLjiYlj3LXIc_X6L2y_wi9pqX183EWYZNh21pUxLFLsN0e29vTRxSkRupyvTDZMKwQvYONlUpbvf04akh9yWnrL6cSwibObSkeJUlfPdQ9UjXiUEg6X4HH2/s640/PMO_7848.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOq9Du0zNanf7UC6yuTZZ1vpLjiYlj3LXIc_X6L2y_wi9pqX183EWYZNh21pUxLFLsN0e29vTRxSkRupyvTDZMKwQvYONlUpbvf04akh9yWnrL6cSwibObSkeJUlfPdQ9UjXiUEg6X4HH2/s72-c/PMO_7848.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/afrika-iandae-rasilimali-watu-kusimamia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/afrika-iandae-rasilimali-watu-kusimamia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy