Na Benny Mwaipaja, WFM, Arusha SERIKALI imesema kuwa itayafanyiakazi maombi ya wastaafu wanaolipwa na Hazina ya kutaka kuongezewa viwa...
Na Benny Mwaipaja, WFM, Arusha
SERIKALI imesema kuwa itayafanyiakazi maombi ya wastaafu wanaolipwa na Hazina ya kutaka kuongezewa viwango vya pensheni wanavyolipwa ili viweze kuwasaidia kukidhi mahitaji yao.
Ahadi hiyo imetolewa Jijini Arusha na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Hazina walioko katika Kanda ya Kaskazini, mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
1. Allen Kijazi-Mstaafu Arusha
2. Kisali Eliya-Mstaafu Arusha
3. Regular Mosha-Mstaafu Arusha
4. Msimbe Mohamed-Mstaafu Arusha
5. Mathew Boniface – Mstaafu Arusha
6. Mwanakombo Yusuph-Mstaafu Arusha
Naibu Katibu Mkuu huyo, Bi. Doroth Mwanyika amesema kuwa maombi ya wastaafu hao hususan wale waliostaafu miaka mingi iliyopita yana mantiki
Doroth Mwanyika-Naibu Katibu Mkuu - Hazina
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Mohamed Mtonga, amesema kuwa zoezi hilo la kuwahakiki wastaafu wanaolipwa na Hazina limelenga kuhuisha taarifa za wastaafu hao
Bw. Mohamed Mtonga- Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Kwa upande wake Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe ameeleza kuwa pamoja na zoezi hilo lililofanyika katika mikoa 11 nchini kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni baadhi ya wastaafu kutokuwa na baadhi ya nyaraka zinazotakiwa
Bw. Stanslaus Mpembe-Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi
Tayari zoezi kama hilo la uhakiki wa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango limefanyika katika Kanda za Pwani na Nyanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo wastaafu zaidi ya elfu 40 wanatarajiwa kuhakikiwa nchi nzima.
COMMENTS