Marehemu Felix Kapinga enzi za uhai wake. Wanajumuia ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys Hig...
Marehemu Felix Kapinga enzi za uhai wake.
Wanajumuia
ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys High
School na Lugalo Secondary School wanasikitika kutangaza kifo cha
aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Felix Kapinga kilichotokea Usiku
wa Tarehe 3/12/2016 katika Hospitali ya Ikonda Mission Mkoa wa Njombe
baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Tunachukua
fursa hii kutoa pole kwa Mke wa marehemu, Mtoto wa marehemu, Mama mzazi
wa marehemu, wafanyakazi wenzake kutoka Njombe community Bank, Ndugu,
jamaa, Marafiki na wana familia kiujumla kwa msiba huu walioupata,
tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mazishi
yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 06/12/2016 huko huko Njombe katika
eneo la kijiji kinachotambulika kwa jina la Ramadhani ambako Mama mzazi
wa marehemu ndiko anakoishi, shighuli za Mazishi zinategemewa kufanyika
kuanzia saa 6.00 Mchana. Kwa taarifa zaidi unaweza ukawasiliana kwa
namba
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.
COMMENTS