Mfanyabiashara Yusuf Manji, akiwa huru wakati anatoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2017. NA K-VI...
Mfanyabiashara Yusuf Manji, akiwa huru wakati anatoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2017.
NA K-VIS BLOG
OFISI ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, (DPP), imeiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam kuwa haina nia ya kuendelea na Kesi ya Uhujumu Uchumi iliyomfungulia Mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Yusuf Manji na kwa maana hiyo Mahakama ikaamua kuifuta kesi hiyo na kumuachia huru Mfanyabiashara huyo.
Pamoja na Manji, pia washtakwia wenzake wawili, nao wameachiliwa huru.
Mkurugenzi wa ashtaka aliwasilisha hati ya kuomba kuondolewa kwa mashitaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, kueleza nia hiyo ya DPP, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Huruma Shaidi, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo aliliondoa na kuwaachia huru washitakiwa hao.
Baada ya kusota rumande kwa miezi kadhaa, leo hii Manji amepata fursa ya kuungana na familia yake na jamaa zake na kabla ya kuachiwa huru, Manji na wenzake waliletwa Mahakamani hapo wakitokea Mahabusu ya gereza la Keko.
Manji alishtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi baada ya kukutwa na vitambaa vya sare za jeshi vyenye thamani ya shilingi milioni 200 pamoaja na mihuri ya jeshi.
“Kama tulivyomzoea Yusuf Manji, ni mfanyabiashara na atarudi na kusimamia shughuli zake za kila siku, uhuru wake ni muhuimu na tunaimani atanednelea na biashara zake.” Alisema wakili wake, Bw. Hudson Ndusyepo.
Mfanyabiashara huyo bado anakabiliwa na kesi nyingine ya matumizi ya madawa ya kulevya ambapo kesi hyo imefikia hatua ya utetezi.
Manji akiwa na wakili wake Bw. Hudson Ndusyepo.
COMMENTS