WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Cyrus Castico akiwa na Mke wa Balozi Mdogo wa C...
MTOTO Ruaba Abdallah Ali akitoa shukrani kwa Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar kwa msaada wake huo, hafla hiyo imeendana na upimaji wa Afya za Watoto hao.
|
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia na kutowa nasaha zake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Upimaji wa Afya kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar zilizotolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina walioko Zanzibar. |
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizundua mpango wa upimaji wa Afya kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar akiwa na Mtoto Yussuf Abdalla (4) akifanyiwa uchunguzi wa afya yake na Daktari Qin Qin. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, uzinduzi huo umefanyika katika makazi yao mazizini Zanzibar |
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua upimaji wa Afya kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar akiwa na Mtoto Yussuf Abdalla (4) akifanyiwa uchunguzi wa afya yake na Daktari Qin Qin, uzinduzi huo umefanyika katika makazi yao mazizini Zanzibar. |
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mtoto Yussuf Abdallah baada ya kuzindua upimaji wa Afya kwa Watoto Yatima wa Mazizini Zanzibar. Kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na kulia Daktari Bingwa wa Watoto kutoka China Dr. Qin Qin. |
MKE wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akiwa na Mtoto Wahida Abdallah akipimwa homa na Daktari Bingwa kutoka China, Dkt.Guoyu Lan. wakati wa hafla hiyo ya uchunguzi wa Afya za Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar |
MADAKTARI Bingwa kutoka China Li Hao na Wang Junguo wakitowa huduma ya kuchunguza Afya za Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizina Zanzibar baada ya uzinduzi huo uliofanya na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, katika makaazi hayo. |
DAKTARI Bingwa kutoka Nchini China, Guoyu Lan akimpima mmoja wa watoto wa Nyumba ya Watoto Mazizini afya yake wakati wa upimaji wa afya zao uliotolewa bure na Ubalozi Mdogo wa China Zanzibar.
|
DAKTARI Bingwa kutoka China, He Qibin akitowa huduma ya kuwapima presha watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar jana. (Picha na Othman Maulid) |
COMMENTS