TPSF YAMWAGA BALOZI WA CHINA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI
HomeJamii

TPSF YAMWAGA BALOZI WA CHINA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing katika hafla fupi ambayo i...

WAZIRI MAKAMBA: MUUNGANO NI URITHI WETU, TU UTUNZE.
CAG MSTAAFU LUDOVICK UTOUH BIL.252/- ZA WIZARA YA UJENZI - DR.MAGUFULI ALISHUTUMIWA KUZITUMIA VIBAYA
CCM ZANZIBAR YAWATAKA WANANCHI KUFUATA MAELEKEZO YA SMZ

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing katika hafla fupi ambayo imefanyika katika hoteli ya Serena iliyopo Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kumuaga, Mwenyekiti wa TPSF, Dk. Reginald Mengi alimshukuru Dk. Youqing kwa mambo yote ambayo ameyafanya akiwa balozi wa China nchini na kumuomba kuendelea kushirikiana na Tanzania hata atakaporejea China.

“Muda mwingine nashindwa kujua kama unaiwakilisha China au Tanzania umekuwa na matendo mema kwa Tanzania kwa kipindi chote ambacho umefanya kazi nchini umekuwa daraja kubwa la kuunganisha China na Tanzania,

“Wote tunajua umuhimu wa biashara ya Tanzanania na China ilivyo kubwa na mambo mambo mengi uliyoyafanya yalifanikiwa, jambo ambalo tunaweza kusema ni tutakukumbuka sana,” alisema Dk. Mengi.

Kwa upande wa Dkt. Lu Youqing aliishukuru (TPSF kwa ushirikiano waliomba kwa kipindi chote ambacho alikuwa akifanyakazi nchini na kuahidi kuwa hata atakaporudi China ataendelea kushirikiana nao.

“Tumeishi vizuri kwa kipindi nilichokuwa hapa niwaahidi kuwa nitarudi tena Tanzania nikiwa kama mfanyabiashara na siku moja ninapenda kuwa mwanachama wa TPSF, kuweni huru kuja hata China kujifunza namna China tunafanya biashara,”alisema Dkt. Youqing.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akisalimia na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Kivukoni uliopo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza katika hafla ya kumuaga Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing. Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla ya kumuaga baada ya muda wake wa kufanya kazi nchini kuisha. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa na viongozi wengine wa TPSF walioshiriki hafla ya kumuaga Balozi Youqing. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa TPSF.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TPSF YAMWAGA BALOZI WA CHINA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI
TPSF YAMWAGA BALOZI WA CHINA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/09/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/tpsf-yamwaga-balozi-wa-china.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/tpsf-yamwaga-balozi-wa-china.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy