AHMED ALBAITY AWASILI NA KUPOKELEWA BEIJING- CHINA
HomeJamii

AHMED ALBAITY AWASILI NA KUPOKELEWA BEIJING- CHINA

 Hatimaye yule mtanzania aliyesaidiwa kupata ufadhili wa matibabu na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amewasili leo h...

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA MACHI 16 DAR ES SALAAM
MASAUNI AZINDUA VITUO MWENDO SITA VYA POLISI, AWAASA WANANCHI KUJIKITA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELE
HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOZINDUWA KIWANDA CHA MOUNT MERU OIL MILLERS, SINGIDA MACHI 11,2018

 Hatimaye yule mtanzania aliyesaidiwa kupata ufadhili wa matibabu na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amewasili leo hii majira ya saa 9:20 alasiri katika Uwanja wa kimataifa wa Beijing Capital. Mtanzania huyo aitwaye Ahmed Albaity alipokekewa na Maafisa waandamizi wa ubalozi pamoja na watanzania waishio hapa jijini Beijing na kusindikizwa kwenye hospitali ya kimataifa ya Puhua.

Ndugu Ahmed Albaity  ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo ambalo limedumu kwa takribani miaka kumi na moja akiwa kitandani,tayari ameanza kupatiwa  Matibabu  katika hatua za  awali  mara tu baada ya kuwasili hospitalini hapo.

Mapema akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakitanzania Wanaosoma na kuishi nchini humo Bw. Remidius Emmanuel ambaye pia ni Katibu Mkuu Shirikisho hilo amesema wao kama watanzania wanaosoma na kuishi katika Taifa la China  wameshiriki kumpokea Mtanzania mwenzao (Ndugu. Ahmed Albaity )  na kwamba  kwa kipindi chote ambacho atakuwepo hapa Beijing China wataendelea kutoa Ushirikiano na kumjulia hali wakati wote.
 "Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU amemuongoza Bw.Ahmed kufika salama hapa Beijing, Tumeshuhudia watanzania wakimsindikiza   uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na  kuongozwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, huu ni upendo wa kipekee, na sisi tumeguswa na kuwiwa kumpokea tukiongozwa na Maafisa waandamizi wa Ubalozi wetu hapa China" Alisema Bw. Remidius.

Kwa upande wake ndugu Ahmed Albaity ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma na kuishi nchini humo kwa moyo wao wa upendo na namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe alioambatana nao.

Bw.Michael Semindu moja kati watanzania wanaosoma nchini humo aliyeshiriki mapokezi hayo  alimhakikishia Ndugu Ahmed Ushirikiano kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu jijini Beijing "Nimefurahi kuungana na Maafisa wa Ubalozi pamoja na watanzania wenzangu kumpokea mwenzetu, tunamuahidi ushirikiano kwa kipindi chote atakachoendelea kupata matibabu  nchini China"  Alisema Bw. Michael

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AHMED ALBAITY AWASILI NA KUPOKELEWA BEIJING- CHINA
AHMED ALBAITY AWASILI NA KUPOKELEWA BEIJING- CHINA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEC-g1x4XIP36f-fysOfYhzVkayNOUEGaBjXMRHmkBckNyvcIbDnHsmDI3qKUDo86eH6jgD93fJ6jkP2A3wkmRerDuLZoUFjck07rDwNgZ35VU0qqCVUW_Hi8vg3Mi7zsfDyO0lQ7ls-M/s400/WhatsApp+Image+2018-03-05+at+17.51.02.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEC-g1x4XIP36f-fysOfYhzVkayNOUEGaBjXMRHmkBckNyvcIbDnHsmDI3qKUDo86eH6jgD93fJ6jkP2A3wkmRerDuLZoUFjck07rDwNgZ35VU0qqCVUW_Hi8vg3Mi7zsfDyO0lQ7ls-M/s72-c/WhatsApp+Image+2018-03-05+at+17.51.02.jpeg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/ahmed-albaity-awasili-na-kupokelewa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/ahmed-albaity-awasili-na-kupokelewa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy