NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM
HomeJamii

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi wa TANESCO alipotembela  mrad...

WAZIRI MKUU AHOJI TANZANIA KUTOKAMILISHA MKATABA WA MAWAKILI
WAZIRI UMMY AZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LEO DAR ES SALAAM
RAIS DKT MAGUFULI AMPIGIA SIMU RC MAKONDA NA KUMPONGEZA KWA KAZI ANAYOIFANYA


 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi
wa TANESCO alipotembela  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20,
2017.
 Naibu Waziri, Mgalu, (katikati),
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka,
(kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendjai wa TANESCO, (anayeshughulikia
usafirishaji umeme), Mhandisi, Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili
kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kigamboni
jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017.
 Wahandisi wa TNESCO wakimalizia
kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo cha Kigamboni.





NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa
Nishati, Mhe. Subira
Mgalu, ameendelea na ziara yake ya kujifunza kwa kukagua miradi mingine miwili
mmoja wa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme Kimbiji na kingine cha kupoza
umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017.
Alhamisi Oktoba
19, 2017, Mhe. Mgalu
alifanya ziara kama hiyo kwa kutembelea vituo viwili vya kupoza umeme vya
Mbagala na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa KIgamboni,
Mheshimiwa Naibu
waziri ambaye alifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya mpya ya Kigamboni,
Bi. Rachel
Mhando, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi
wengine wa juu wa Shirika hilo, alianza kwa kukagua kituo cha Kigamboni ambapo
aliwakuta mafundi wa TANESCO wakimalizia kufunga mitambo kwenye kituo
hicho.
Aidha Naibu waziri
alimalizia ziara
yake kwa kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji ambapo kazi ya
kusafisha eneo la ujenzi nayo imekamilika na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa
vifaa ili ujenzi uanze.
Mheshimiwa Mgalu
alisema kutokana na
ongezeko kubwa la watumiaji wa umeme, vituo hivyo vitasaidia sana kuboresha
huduma ya upatikanaji umeme hususan katika kipindi hiki ambacho serikali ya
awamu ya tano imejielekeza kujenga uchumi wa viwanda na hitajio kubwa katika
utekelezaji wa mpango huo ni upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Niwashukuru tu
kwa ksuema, ziara
yangu hii ni ya kwanza kwenye eneo hiki tangu niteuliwe na nimeona nije ili
nijionee jitihada hizi za kuboresha hali ya umeme wilayani Kigamboni ambapo
kuna uhitaji mkubwa wa umeme ,kutokana na ongezeko kubwa la watu.”
Alisema.
Akieleza zaidi
Mheshimiwa Mgalu
alihimiza Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambalo kwa niaba ya serikali ndilo
linatekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili hatimaye wananchi wapate
huduma ya umeme katika hali bora zaidi.
Aidha Katibu
Tawala wa Wilaya ya
Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, Aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika
wilaya hiyo na kusema serikali wilayani Kigamboni itatoa kila aina ya msada ili
kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika.
“Hii ni wilaya
mpya ni jambo la
kushukuru kuwa katika kipindi kifupi wilaya inaletewa mradi mpya wa kuboresha
umeme kwa kweli wananchi wana matarajio makubwa na mradi huu na sisi
tumefarijika sana.” Alisema Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni.






 Naibu waziri akipatiwa maelezo
na Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi
Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu waziri akipatiwa maelezo
na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji
umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito
Mwinuka.
 Naibu waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu, (kushoto), akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Wilaya
ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa
wilaya hiyo kuanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya
umeme vya Kigamboni na Kimbiji.
 Meneja
Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi
Mahende Mgaya, (kulia), akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa
Nihstai, Mhe. Subira Mgalu, (wakwanza kushoto) kwenye eneo la ujenzi
wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Kimbiji, wilayani
Kigamboni jijini Dar es Salaam, Oktoba 20, 2017.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Temeke, Mhandisi Jahulula, (kulia), akimuonyesha mchoro wa kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu, (katikati), na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi.
Rachel Mhando, wakati Mhe. Mgalu alipotembekea kituo hicho
leo.
 Mhe. Mgalu akizungumza jambo.
Picha ya pamoja mwishoni mwa ziara.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM
NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgt34oQw9uV1InUMPg65-j0Ls5vxXYtr1NzB4QERfzaUdB4PL9BDm9hdiVWwEkYlPgah6az0cbVccHqkNEObWa_w3OsMSeVm9OwA_YD4Xy4mNiKp0u6awGHndMK-WzgDGV_-JwJgRneWiCC/s640/DSC_7777.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgt34oQw9uV1InUMPg65-j0Ls5vxXYtr1NzB4QERfzaUdB4PL9BDm9hdiVWwEkYlPgah6az0cbVccHqkNEObWa_w3OsMSeVm9OwA_YD4Xy4mNiKp0u6awGHndMK-WzgDGV_-JwJgRneWiCC/s72-c/DSC_7777.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-wa-nishati-subira-mgalu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-wa-nishati-subira-mgalu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy