Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea jambo wakati wa kongamano la pili la maj...
Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa taasisi hiyo Profesa Godwin Mjema na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Godwin Mjema akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi. Segolena Francis akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) Jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Utafiti kutoka Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT),akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi (wanne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi mara baada ya kufungua kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) Septemba 5 jijini Dar es Salaam.
COMMENTS