SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
HomeJamii

SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma ...

MHE. LUGOLA AFANYA ZIARA TANDALE KWA MTOGOLE NA KUZINDUA OPERESHENI YA MIEZI MIWILI YA KUSAFISHA MITO NCHI NZIMA
DKT. FAUSTINE NDUGULILE AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA CHAMA CHA WATAALAMU WA MAGONJWA YA FIGO MJINI DODOMA
WAFANYAKAZI 143 WA OFISI YA RAIS UTUMISHI WAHAMIA DODOMA AWAMU YA PILI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Selemani Jaffo na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.

Baadhi ya Washiriki wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu, kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo na amemtaka kila mdau wa lishe aonyeshe bayana mchango wake katika kukabiliana na utapiamlo nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akifungua mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Pia alizindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 (Joint Multisectoral Nutrition Review).

“Viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali wabaini kiwango cha utapiamlo katika maeneo yao, waonyeshe mbinu za kukabiliana na hali hiyo, wafanye tathmini ya ufanisi na watoe taarifa za ufanisi,” amesema.


Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote, wahakikishe shilingi 1,000 ambazo Halmashauri zilielekezwa kutenga kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano, zinatolewa na kutumika kama ilivyopangwa.


“Tulikubaliana kila Halmashauri lazima ikusanye makusanyo ya ndani kwa asilimia zaidi ya 80. Nilisema kiwango cha chini kisipungue asilimia 80. Na kupitia makusanyo hayo, ndipo tunapata fedha za kutenga kwa masula kama haya,” alisisitiza.


“Napenda kusisitiza kwamba ni lazima tufanye tathmini ya wapi tumefikia na wapi tumekwama katika kupambana na tatizo la utapiamlo hapa nchini,” alisema.


Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanaisimamia mikoa na halmashauri zao kutekeleza afua zilizoainishwa katika Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwa kuzijumuisha katika mipango yao na kuzitengea fedha kwenye bajeti zao za kila mwaka.


Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema amefurahishwa sana na kaulimbiu ya mkutano huo isemayo “Lishe Bora: Msingi wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania” ambayo kimsingi inaendana na dhamira yetu ya kujenga uchumi wa viwanda kama kichocheo cha mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.


Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wadau wawekeze kwenye viwanda vya usindikaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuongeza wingi wa vitamini na madini katika vyakula na hatimaye kuboresha lishe na afya ya jamii. “Napenda kusisitiza kuwa Serikali imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo tutumie fursa hii kikamilifu,” aliongeza.


Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema kuna baadhi ya Halmashauri na mikoa hazijaunda Kamati za Afua za Lishe.

“Ninaomba Halmashauri na mikoa ikamilishe kuunda kamati za mikoa na pia watendaji wahakikishe fedha zimetengwa na zinatolewa. Lakini cha msingi ni kwamba fedha hizi zitumike kwa matibabu ya utapiamlo na masuala ya lishe na si vinginevyo,” alisisitiza.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
L. P. 980,
40480 DODOMA,
ALHAMISI, SEPTEMBA 7, 2017.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh49HUajitW3SxRSs-IVbDRM9fKGWhCDVxal8jGUuQtFMWnyVkVxBI1gp5xq074X30pFj5CbxtaDJFeT4EnIc-_xE3098tB-QP8GO2eDXMSplz_nxOVNgyiFqirdtVTZqsPgb0rjkSwJcMk/s640/PMO_0045.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh49HUajitW3SxRSs-IVbDRM9fKGWhCDVxal8jGUuQtFMWnyVkVxBI1gp5xq074X30pFj5CbxtaDJFeT4EnIc-_xE3098tB-QP8GO2eDXMSplz_nxOVNgyiFqirdtVTZqsPgb0rjkSwJcMk/s72-c/PMO_0045.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/serikali-yatenga-shbilioni-11-kukabili.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/serikali-yatenga-shbilioni-11-kukabili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy