Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama Mh. Jenista Mhagama (katikati) akifungua mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mw...
Mwenyekiti
wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama Mh. Jenista Mhagama (katikati)
akifungua mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa
uzazi salama
Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ), Bi. Sizarina Hamisi
(mbele) akiwasilisha mada katika mkutano kati ya WRATZ na kundi la
Wabunge wa uzazi salama mjini Dodoma
Mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salama ukiendelea.
WABUNGE
wa kundi la uzazi salama wametakiwa kuhamasisha na kutetea Bajeti ya
Afya ya Uzazi na Mtoto ili ipewe kipaumbele katika mipango ya
Halmashauri kwa mwaka 2017/2018.
Hamasa
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama, Mh.
Jenista Mhagama wakati akifungua mkutano uliowakutanisha wabunge wa
kundi hilo wapatao 30 pamoja na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama
(WRATZ) mjini Dodoma kujadili kuhusu mchango wa wabunge katika
kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akiwasilisha
mada katika mkutano huo Meneja mradi wa Muungano wa Utepe mweupe
(WRATZ) Bi Sizarina Hamisi alisema kwa mujibu wa takwimu ya Idadi ya
Watu na Afya Tanzania ya mwaka 2015-2016 zinaonyesha kuwa kwa sasa
wakina mama 30 na watoto wachanga 180 wanapoteza maisha kila siku
kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi.
Kwa
upande wao baadhi ya wabunge wamekiri kuwa pamoja na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na serikali bado vifo vya mama na mtoto
vitokanavyo na uzazi ni changamoto hivyo kuna haja yakuongeza jitihada
ili kutatua tatizo hilo ikiwemo bajeti ya afya ya mama na mtoto hasa
huduma za muhimu na dharura kupewa kipaumbele kuanzia ngazi za
halmashauri mpaka serikali kuu.
COMMENTS