DKT. MPANGO AENDELEA NA KAMPENI YA "TITFOTAT NA EFDs" SASA YUKO MKOANI DODOMA
HomeJamii

DKT. MPANGO AENDELEA NA KAMPENI YA "TITFOTAT NA EFDs" SASA YUKO MKOANI DODOMA

BENNY MWAIPAJA, DODOMA WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza "Titfotat na EFDs", katika mi...

MBINU HIZI ZITAKUSAIDIA KUKABILIANA NA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM
MAJALIWA AWASILI MAURITIUS KUMWAKILISHA JPM KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA KIUCHUMI BARANI AFRIKA
TANESCO YATOA TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME MAENEO YA KIBAMBA, MBEZI NA KIMARA



BENNY MWAIPAJA, DODOMA
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza "Titfotat na EFDs", katika mitaa ya mji wa Dodoma leo Julai 27, 2017 na kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatumii ipasavyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi ya Serikali-EFDs na kuwaonya wafanyabiashara kote nchini kuacha mchezo huo.
Dkt. Mpango aliyeambatana na baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini-TRA mkoa wa Dodoma amebaini baadhi ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu hawatoi risiti huku wengine wakiandika kiwango kidogo cha fedha kwenye risiti hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara aliyekumbana na mkono wa Waziri Dokta Mpango, ni Bwana ISDORI SHIRIMA ambaye amekiri kufanya makosa ya kutotumia mashine hizi ipasavyo
“naomba unisamehe Mheshimiwa, sitarudia tena unajua sisi vijana tunabangaiza, lakini nimebaini nimefanya makosa” aliomba msamaha Bw. Shirima
Hata hivyo Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA mkoa wa Dodoma, kufanya ukaguzi wa kina wa mahesabu ya mfanyabiashara huyo ili kubaini kiwango cha kodi alichokwepa na kumchukulia hatua stahiki.


Aidha, Dokta Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Dodoma kuwapeleka ofisini kwake mawakala wote mkoani humo wanaosambaza mashine za kieletroniki za kukusanyia mapato EFDs baada ya kubaini kuwa zaidi ya mashine 100 zimeharibika na hazitumiki tangu jana.


“Kuna kitu sikielewi na hakiingii akilini, inakuwaje mashine ziharibike kwa kiwango hicho, mashine 100 kuharibika kwa siku mbili ni nyingi na ina maana nimekosa mapato mengi” alielezea kwa masikitiko Dkt. Mpango.


Aliagiza mawakala wote wanaosambaza ama kuuza mashine hizo wakutane naye ofisini kwake mjini humo ili kubaini tatizo na kuongeza kuwa haiwezekani wafanyabishara walipie mashine hizo zaidi ya mwezi uliopita lakini hawapelekewi hali inayozidi kuikosesha Serikali mapato yake.


Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamepongeza uamuzi wa Serikali wa kulivalia njuga suala la kodi na kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kutoa risiti wanapouza bidhaa na kudai risiti zenye viwango sahihi vya manunuzi waliyoyafanya ili kuijengea Serikali uwezo wa kuihudumia jamii.


Dokta Mpango ametembelea pia baadhi ya vituo vya mafuta mjini humo na kuwakumbusha wamiliki wote wa vituo vya mafuta kuzingatia agizo la Serikali linalowataka wafunge mashine maalumu za kielektroniki zinazofungwa kwenye pampu za mafuta ndani ya siku 14 ambazo ziko ukingoni.



Kiongozi wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.



Mfanyabiashara wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka lake na kubaini kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti ya mteja aliyenunua tanki la kuhifadhia maji katika moja ya duka linalouza vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi kukagua risiti zao ili kubaini kama kiwango kilichoandikwa kinalingana na kiasi kilichoandikwa kwenye risiti.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti na kupata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Kituo cha Mafuta cha ORYX mjini Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin, alipofanya ziara ya kushitukiza kuangalia kama vituo vya mafuta mjini humo vimefungwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti kwa wateja wao.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa katika mitaa ya mji wa Dodoma alipofanya ziara ya kushitukiza, “titfotat na EFD” kukagua matumizi ya mashine za kutolea risiti kwa njia ya kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara wa maduka mjii humo Julai 27, 2017.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuagiza Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Ngaka Magere, kumkutanisha na mawakala wanaosambaza mashine za kieletroniki za kutolea risiti mkoani humo baada ya kutoridhishwa na huduma zao




Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo ya matumizi ya mashine za kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi wa Kituo kimoja cha Mafuta mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza kituoni hapo kuangalia matumizi ya mashine hizo.


(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WFM)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. MPANGO AENDELEA NA KAMPENI YA "TITFOTAT NA EFDs" SASA YUKO MKOANI DODOMA
DKT. MPANGO AENDELEA NA KAMPENI YA "TITFOTAT NA EFDs" SASA YUKO MKOANI DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1PPlBb9YJjkD_dfyO6P8x_CXRM1pPxzcCcuvTA4k7Giav-CNuTCVeXQdp5b4yT-BdctRqH5UFGZg5WGe9sAW5GQAk_-Hm-aZZjdYnnyjPMCareUxn_iAwEg1ALrdhJowQuwZW9vAlLfU7/s640/IMG_4550.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1PPlBb9YJjkD_dfyO6P8x_CXRM1pPxzcCcuvTA4k7Giav-CNuTCVeXQdp5b4yT-BdctRqH5UFGZg5WGe9sAW5GQAk_-Hm-aZZjdYnnyjPMCareUxn_iAwEg1ALrdhJowQuwZW9vAlLfU7/s72-c/IMG_4550.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/dkt-mpango-aendelea-na-kampeni-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/dkt-mpango-aendelea-na-kampeni-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy