MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA  VYA  UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5
Picha ya pamoja ya watumishi wa Hospitali ya Muhimbili wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto uliofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam.
HomeJamii

MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA VYA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5

NA WAMJW-DAR ES SALAAM HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba viwili vya upasuaji wa ...

WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA II KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO
JESHI LA ZIMAMOTO LAFANYA TAMASHA LA UTOAJI ELIMU KWA UMMA

NA WAMJW-DAR ES SALAAM
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 kutoka Taasisi binafsi ya Archie Wood Foundation ya Scotland ili kufanya huduma hiyo kupatikana kw urahisi nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto uliofanyika  leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa msaada huo umeonyesha jinsi gani Wahisani wana ushirikiano na Serikali katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya afya nchini.
“ Kutokana na Wahisani kujitokeza mara kwa mara katika kushirikiana na Serikali yetu  kwenye sekta ya afya tumepunguza asilimia 40 ya wagonjwa wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu na lengo letu ni kupunguza asilimia 70 mpaka kufikia 2025”alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa Wazazi na walezi  wawe msatari wa mbele kuwakatia watoto wao bima ya afya ijulikanayo kama Toto Afya kwa gharama ya shilingi elfu 54 ili kuokoa gharama zingine zisizo na lazima kwa ajili ya kupata matibabu.
Mbali na hayo Waziri Ummy asisitiza Uongozi na Wataalam wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili kujiridhisha kwa kina ndipo kutoa Rufaa kwa wagonjwa wanaohitajika kutibiwa nje ya nchi wakati wa uzinduzi wa vyumba viwili vya upasuaji wa watoto .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Laurence Museru amesema kuwa kutokana na msaada wa vifaa hivyo Hosiptali hiyo inatimiza idadi ya vyumba viwili vya upasuaji vilivyokamilika kwa ajili ya upasuaji wa watoto.
“Tulikua tunafanya upasuaji kwa watoto wadogo mara tatu kwa wiki kutokna na ufinyu wa vifaa lakini kutokana na vifaa hivi tutafanikiwa kufanya upasuaji mara kumi kwa wiki” alisema Prof. Museru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili Prof. Laurence Museru akitoa maelekezo mbele ya Waziri wa Afya,MaendeleoyaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika wodi ya watoto, wakwanza ni mzazi wa mtoto Patrick Jafari Juma anaesumbuliwa na maradhi (Hayupo kwenye picha).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na mama mzazi wa mtoto Patrick Jafari Juma pindi akitembelea wodi za watoto katika Hospitali ya Muhimbili mapema leo wakati wa uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto.


Watumishi wa Hospitali ya Muhimbili wakifuatilia kwa ukaribu uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto uliofanywa mapema leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha)

Sir Lan Wood kutoka Archie Wood Foundation akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto uliofanyika mapema leo katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili Prof. Laurence Museru akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto. Kulia ni Sir Lan Wood kutoka Archie Wood Foundation.


















Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA VYA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5
MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VIPYA VYA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA BIL.1.5
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvktIC-S-IaeuQVCP-cs4WH-ER5_0NwLgcA2QA7qEeIXqzq_aK02qX4A_MmE8VDCkTE4WZnVHqdqrb8sZZH2ms9h2OeGfqnKnQP9hmyr0PkBpE57gLlXl22MPUu596Bb5DlUbdq7fYrB4/s640/%25231.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvktIC-S-IaeuQVCP-cs4WH-ER5_0NwLgcA2QA7qEeIXqzq_aK02qX4A_MmE8VDCkTE4WZnVHqdqrb8sZZH2ms9h2OeGfqnKnQP9hmyr0PkBpE57gLlXl22MPUu596Bb5DlUbdq7fYrB4/s72-c/%25231.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/muhimbili-yapokea-msaada-wa-vifaa-vipya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/muhimbili-yapokea-msaada-wa-vifaa-vipya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy