WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA II KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Tanga, watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijiji (REA) hawapo pichani.

HomeJamii

WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA II KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya usamba...

SERIKALI YAMJIBU TUNDU LISSU
UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI WA AWAMU YA PILI KUFANYIKA MWEZI AGOSTI, 2017
MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI: ACP MULIRO ALETWA KINONDONI

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Pili  (REA II) watachukuliwa hatua za kisheria na Serikali.
Mgalu ameyasema hayo  tarehe 22 Desemba, 2017 katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam katika kikao chake na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Tanga inayosimamiwa na  Wakala wa Nishati Vijijini
Wakandarasi hao ni pamoja na kampuni ya Derm inayosambaza miundombinu ya umeme katika  wilaya za Handeni, Kilindi, Korogwe na Lushoto,  Kampuni za Radi, Njarita na Aguila zinazosambaza umeme katika  wilaya za Mkinga, Pangani, Muheza na Bumbuli na kampuni ya Namis Cooperate Ltd inayosambaza miundombinu ya umeme katika wilaya zote za Tanga.
Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Naibu Waziri Mgalu, alisema kuwa wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia REA Awamu ya Pili walilipwa malipo karibia yote hivyo walipaswa kukamilisha miradi yote kwa wakati.
Aidha, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu kuongeza kasi katika miradi ya usambazaji wa umeme vijijini na kuongeza kuwa kipaumbele kitolewe katika taasisi kama Shule, Vituo vya Afya, zahanati, Visima vya Maji ili wananchi waanze kufurahia  huduma za jamii.
Vilevile aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA katika mikoa miwili tofauti kuhakikisha kuwa kasi inakwenda kwa kiwango sawa na kuepuka kuwekeza nguvu kwenye mkoa mmoja tu.
“ Kwa wakandarasi wanaosambaza miundombinu ya umeme katika mkoa zaidi ya mmoja lazima wahakikishe  kasi inakwenda sawa kwa mikoa yote, pasiwepo na mkoa ambao mradi wake unakamilika mapema huku mkoa mwingine ukiwa nyuma kabisa,” alisisitiza Mgalu.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mgalu alitoa tahadhari kwa wakandarasi watakaobainika wanaingiza nguzo  za umeme na tranfsoma nje ya nchi tofauti na maelekezo yaliyotolewa awali kuwa vifaa vyote vya ujenzi wa mradi wa umeme vitoke hapa nchini
Alisema Serikali ilishakutana na wadau wa vifaa ikiwamo wasambazaji wa Nguzo za Umeme na kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha TANALEC kilichopo jijini Arusha na kujiridhisha uwezo wa wadau hao katika usambazaji wa vifaa.


Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)katika mkoa wa Tanga, watendaji kutoka Wizara ya Nishati,  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani)





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA II KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
WAKANDARASI WALIOSHINDWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA II KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5RMU_c9Ew3mszdlN3mlrKihImf1E8YJeawpfBQXA0BFURWk5DEEifyLKMaj9x8swUAic-tVGTWjjMhDnzZTNMEn8bwVFdR3Vy0t8ewfqUXDJ6OPNGVD4ElsTuqG9OLThIY5Lebo98rA0/s640/Picha+Na+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5RMU_c9Ew3mszdlN3mlrKihImf1E8YJeawpfBQXA0BFURWk5DEEifyLKMaj9x8swUAic-tVGTWjjMhDnzZTNMEn8bwVFdR3Vy0t8ewfqUXDJ6OPNGVD4ElsTuqG9OLThIY5Lebo98rA0/s72-c/Picha+Na+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wakandarasi-walioshindwa-kukamilisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wakandarasi-walioshindwa-kukamilisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy