RAIS MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI ARUSHA
HomeJamii

RAIS MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI ARUSHA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz T...

HOJA YA HAJA: UTANDAWAZI WA UCHUMI NCHINI TANZANIA
WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA YAKE MDOGO MHE JAKAYA KIKWETE
WABUNGE WAPAZA SAUTI KUHUSU UZAZI WA MPANGO, KUPUNGUZA VIFO VINAVYOTAKANA NA UZAZI NA KUPANGA MAENDELEO TAIFA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Septemba, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.
Akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Sangsi nje kidogo ya Jiji la Arusha na wananchi wa Pacha ya Kia Mkoani Kilimanjaro na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za wananchi na kuwahudumia bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za kisiasa, dini na ukabila.
Mhe. Rais Magufuli amesema katika kutimiza azma hiyo Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Usa River  – Arusha inayojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 139, mradi wa maji wa Arusha utakaogharimu Shilingi Bilioni 42, mradi wa kusambaza umeme katika vijiji zaidi ya 200 na mingine mingi inayotekelezwa katika maeneo hayo.
“Nina uhakika nyinyi wakazi wa Arusha mnaona Arusha inavyobadilika, kabla ya kujengwa barabara hii kulikuwa kunatokea ajali nyingi, na kuna watu walikufa pale kwenye daraja, inawezekana wengine wameanza kusahau, wanaozaliwa sasa hivi wanaweza kuona haya sio chochote lakini hii ni ishara ya kupanda kwa uchumi wetu, uchumi unapopanda na miundominu inakuwa mizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wakiwemo wafanyakazi ambao wamelalamikia kuhamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao na amerejea agizo lake la kupiga marufuku mfanyakazi yeyote kuhamishwa kituo cha kazi pasipo kulipwa stahiki zake.
Kuhusu kero za wananchi wa pacha ya Kia waliolalamikia tatizo la uhaba wa maji, kunyang’anywa maeneo ya biashara na waliokuwa walinzi wa uwanja wa ndege kudai haki zao Mhe. Rais Magufuli ameziagiza mamlaka husika kushughulikia matatizo hayo.
Mhe. Rais Magufuli amerejea Jijini Dar es Salaam.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Arusha

25 Septemba, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Singisi kata ya Akeri nje kidogo ya jiji la Arusha kwenye njia panda ya KIA waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kurejea Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.




Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira na wa Arusha Mhe Mrisho Gambo wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira kabla ya  kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kabla ya kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungiwa mikono na Mkuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati ndege yake ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  baada ya kumsindikisza Rais Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha. (Picha na IKULU)












Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI ARUSHA
RAIS MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI ARUSHA
https://lh3.googleusercontent.com/0RWCkEBPYNgyIwwKx9IZNm_nEyI6tiiXON2LgCdSYEjPrCPglIs_y-CQlO-aJuwr2e_nqFSpbjZGYElcG3c5bUm4eaEccj4NMF6LtHrcdaEsPLJg1tQ3rsmuvLZ6Bxh3GUMql4HpiLNqlTgAug
https://lh3.googleusercontent.com/0RWCkEBPYNgyIwwKx9IZNm_nEyI6tiiXON2LgCdSYEjPrCPglIs_y-CQlO-aJuwr2e_nqFSpbjZGYElcG3c5bUm4eaEccj4NMF6LtHrcdaEsPLJg1tQ3rsmuvLZ6Bxh3GUMql4HpiLNqlTgAug=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-magufuli-amaliza-ziara-ya-siku-6.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-magufuli-amaliza-ziara-ya-siku-6.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy