Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na moja ya wahudumu wa Choo Cha Kituo Cha Mabasi Simi 2000 Mara ba...
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na moja ya
wahudumu wa Choo Cha Kituo Cha Mabasi Simi 2000 Mara baada ya ziara ya
kushitukiza kujionea Hali ya ukusanyaji mapato.





Na Mwandishi Wetu, Dar as salaam
Afisa
Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg Fulgence Rweyagaza
ametakiwa kujitathmini Kama anafaa kuendelea na majukumu yake ama
vinginevyo kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya
Manispaa katika Kituo Cha Mabasi Simu 2000 kilichopo Kata ya Sinza.
Agizo
Hilo limetolewa Jana June 23, 2017 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo
Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato isivyo na weledi.
MD
Kayombo amebaini kutotolewa risiti ipasavyo ambapo Jambo Hilo limetajwa
kuwa ni moja ya sababu ya kupatikana mapato kiduchu ukilinganisha na
huduma zinazotolewa Kwa wananchi.
Akiwa
kituoni hapo MD Kayombo aliamua kutumia zaidi ya masaa matano kusimama
mwenyewe dirishani kukusanya fedha za watu waliokuwa wanapatiwa huduma
ya Choo ambapo kwa muda wote huo amebaini uwepo wa fedha nyingi ambazo
zilikuwa zinapotea.
Kituo Cha mabasi cha Simu 2000 kina maeneo matatu ya ukusanyaji mapato ambapo ni Choo, Soko pamoja na Daladala.
Katika
hatua nyingine MD Kayombo amewafuta kazi watumishi wawili wa kujitolea
ambao wamekosa sifa ya kuendelea kuwa wasaidizi katika kazi za Kituo
hicho.
COMMENTS