Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimvisha nembo ya kijani Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalu...
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimvisha nembo ya
kijani Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha
Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kwa niaba ya wahitimu wenzake. Mafunzo
hayo Maalum yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya
Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini
Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba fupi
kwa Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza
Kozi Namba 11 kabla ya kuyafunga rasmi leo Januari 13, 2017.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa
maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo hayo.
Askari
Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi
Namba 11 wakiingia uwanjani kwa ajili ya kutoa maonesho mbalimbali ya
Ukakamavu na ujasiri.
Onesho
Maalum la Ukakamavu na ujasiri kama inavyoonekana katika picha Askari
wa Kikosi Maalum akihimiri kipigo cha nyundo katika mwili wake kwa
ujasiri wa hali ya juu.
Askari
Wahitimu wa Mafunzo hayo Maalum wakionesha umahiri wao wa kuvuka
vikwazo mbalimbali kwa kutumia kamba kama inavyoonekana katika picha.
Wahitimu wa Mafunzo Maalum wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) akipokea Salaam ya
heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na askari
wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi
Namba 11. Hafla ya hiyo imefanyika leo Januari 13, 2017 katika Viwanja
vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga,
Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo
Dkt. Juma Malewa .
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akikagua Gwaride
Maalum la heshima lililoandaliwa na Askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya
Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kama inavyoonekana
katika picha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) akimtunuku cheti
cha sifa Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha
Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 ambapo Mafunzo hayo yamefungwa rasmi
leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza
Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Jeshi la Magereza).
COMMENTS