CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea urais wa Kenya kupitia chama tawala cha Jubi...
CHAMA
Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea
urais wa Kenya kupitia chama tawala cha Jubilee, Rais wa sasa Uhuru Kenyatta.
Akitangaza
uamuzi huo wa chama, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema leo Mei 27,
2018 kuwa Baraza Kuu la chama hicho lililoketi leo mjini Dodoma, lemeamua kwa
kauli moja kumuunga mkoro Rais Kenyatta, kutokana na kukuza demokrasia ya vyama
vingi nchini humo.
“
Lakini pia Rais Kenyatta ameturidhisha kutokana na sera zake za kiuchumi ambazo
zimeifanya Kenya kusonga mbele kiuchumi.” Alisema Mbowe.
Kenya
itafanya uchaguzi wake Mkuu mwezi Agosti mwaka huu 2018 ambapo Rais Kenyatta
anatetea kiti hicho akichuana na mgombea wa upiznani, Raila Udinga.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akizungumza kwenye kikao hicho

COMMENTS