TAARIFA KUHUSU JPC KATI YA TANZANIA NA UGANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa (wa pili kushoto) wakiweka saini Nyaraka yenye maelezo ya masuala yote yaliyokubaliwa katika kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda

HomeJamii

TAARIFA KUHUSU JPC KATI YA TANZANIA NA UGANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kute...

MDAHALO WAKUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII
TRA YATAMBUA UMUHIMU WA WAANDISHI WA MTANDAO KATIKA KUFIKISHA ELIMU KWA MLIPA KODI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Kikao cha JPC kati ya Tanzania na Uganda chafunguliwa jijini Arusha


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA NA UGANDA ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA
Tanzania na Uganda zimefungua sura mpya ya ushirikiano baada ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo kusaini nyaraka inayoainisha maeneo mbalimbali ambayo nchi hizo zimekubali kushirikiana kwa pamoja ili kuinua uchumi wa mataifa yao.
Nyaraka hiyo iliyosainiwa leo jijini Arusha imetokana na Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)  kati ya Tanzania na Uganda kilichofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 03 Aprili 2017.

"Makubaliano haya yataongeza chachu ya uhusiano na ushirikiano wetu na Uganda, japokuwa tulichelewa kufanya kikao cha JPC tokea mkataba uliposainiwa mwaka 2007 nchini Uganda". Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alisema alipokuwa akisoma hotuba ya kufunga.

Kikao cha JPC kilifanyika kwa kuzingatia makundi ya kisekta ambapo katika kila kundi, wajumbe waliainisha maeneo yenye maslahi kwa pande zote ambayo yanajumuisha pamoja na mambo mengine: uendelezaji wa miundombinu; kilimo; viwanda; biashara; uwekezaji; nishati; utalii; utunzaji wa mazingira; uvuvi; ufugaji; afya; elimu; utangazaji; madini na masuala ya kijamii.

Kikao hicho kilitarajiwa kuhitimishwa kwa kusainiwa mikataba sita lakini kutokana na mashauriano ya ndani ya baadhi ya mikataba kutokamilika, mikataba miwili ndio iliweza kusainiwa. Mikataba hiyo ni ushirikiano katika kuendeleza mradi wa Umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo na huduma za usafiri wa anga.

Mikataba  minne iliyosalia ambayo inahusu ushirikiano katika usafiri wa reli, usafiri wa majini; utangazaji na ulinzi wa raia itasainiwa wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika hivi karibuni hapa nchini.

Waziri Mahiga alieleza kuwa kusainiwa kwa  mikataba hiyo ni muhimu kwa kuwa itaimarisha zaidi misingi ya mahusiano yetu, hivyo alizihimiza pande zote kukamilisha mashauriano hayo ili mikataba hiyo iweze kusainiwa katika muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Uganda kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua uchumi kwa madhumuni ya kuwaondolea umasikini wananchi.

Alisema mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ni moja ya miradi itakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi, hivyo alisisitiza umuhimu wa kukamilisha taratibu zote zilizosalia ili ujenzi huo uweze kuanza.

Alihitimisha hotuba yake kwa kuzipongeza Tanzania na Uganda kwa kufanikisha uwekaji saini wa mikataba miwili ukiwemo wa kuendeleza mradi wa Umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo ambao ulikuwa katika majadiliano kwa zaidi ya miaka minane.

Kikao hicho cha JPC kimefanyika kufuatia maelekezo ya Marais wa nchi hizo waliyoyatoa wakati wa ziara ya Rais wa Uganda nchini mwezi Februari 2017. Viongozi hao waliagiza kikao cha JPC kifanyike kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao ulipangwa kufanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 06 Aprili 2017.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, 05 Aprili, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakiweka saini Mkataba ambapo Tanzania na Uganda zitashirikiana kuendeleza mradi wa umeme wa kutumia maji wa MW 14 katika eneo la Kikagati/Murongo



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAARIFA KUHUSU JPC KATI YA TANZANIA NA UGANDA
TAARIFA KUHUSU JPC KATI YA TANZANIA NA UGANDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJy2RBJrNFsng-8QPPcM5cMdYSID6uXbBGuZodt2_pSyRhR4WlTo7kwhYZ25_eexOHqnhePNX0W-Jy2L2bbF_YnGfDCWGPFAW00Zw8mUMF7ir8GKA8aHiO8WStE0HjJmao65ebOuQWYsk/s640/MAHIGA+NA+JPC.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJy2RBJrNFsng-8QPPcM5cMdYSID6uXbBGuZodt2_pSyRhR4WlTo7kwhYZ25_eexOHqnhePNX0W-Jy2L2bbF_YnGfDCWGPFAW00Zw8mUMF7ir8GKA8aHiO8WStE0HjJmao65ebOuQWYsk/s72-c/MAHIGA+NA+JPC.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/taarifa-kuhusu-jpc-kati-ya-tanzania-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/taarifa-kuhusu-jpc-kati-ya-tanzania-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy