WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga (kushoto) na Mkurugenzi wa ufundi na huduma Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Bengiel Msofe wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Wadau wanaotekeleza Mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma.
HomeJamii

WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII

Na Zuena Msuya, Dodoma Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba (7) kutoka Wizara ya Nishati watakaoshirikiana ...

SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI
MKUTANO WA UWEKEZAJI WA AFRIKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU
MKUCHIKA APONGEZA MCHANGO WA TASAF KATIKA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.

Na Zuena Msuya, Dodoma

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba (7) kutoka Wizara ya Nishati watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa REA III katika kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha utekelezaji wa Mradi huo kwa ufanisi.
Dkt. Kalemani alifanya uteuzi huo baada ya kufanya mkutano na Wadau mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA III wakiwemo, Wakandarasi,  Wawekezaji wenye Viwanda vya kutengeneza miundombinu ya umeme kama vile Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme, Mameneja wa Kanda na Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi nzima.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu pamoja na changamoto zinazojitokeza  katika utekelezaji wa Mradi huo.
Dkt. Kalenani alisema Wahandisi walioteuliwa watashirikiana na Wakandarasi wa REA III kutafanya kazi mbalimbali pamoja na kuwa na mpango kazi wa kila wiki wa kila Mkandarasi katika eneo husika ili kusisimamia kwa ukaribu utekelezaji wake.
Pia watarahisisha mawasiliano yamoja kwa moja kutoka kwa wakandarasi hao na Wizara ya Nishati  ili kufahamu hatua waliofikia na changamoto watakazokuwa wakikabiliana nazo kwa Lengo la kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Awali akizungumza katika mkutano huo Dkt.Kalemani aliwataka wakandarasi hao kutumia busara na uzalendo zaidi katika kuwaunganisha Wananchi na Huduma ya Umeme Vijiji kupitia Mradi wa REA III.
Alifafanua kuwa mbali na kuwepo kwa mikataba inayawaongoza wakandarasi hao kutekeleza majukumu yao, lakini Kuna maeneo ambayo wanapaswa kuyafikia pasipo kuangalia makubaliano ya mkataba.
" Nawasihisi Sana wakandarasi mtumie burasa na uzalendo kuunganisha Wananchi kwa mfano utakuta Kijiji kina Shule au Zahanati  lakini hakuna umeme ila kimepitiwa na mradi wa umeme lakini kijiji hicho hakipo kwenye orodha ya vile vijiji mlivopewa katika mkataba, nawasihi sana kwa hili,tumieni  busara, najua inawezekana kuunganisha ili Watanzania wenzetu wapate huduma Bora za afya au watoto wetu wapate mazingira mazuri ya kujisomea", alisema Dkt. Kalemani
Aidha aliwataka Wakandarasi hao kuendelea kutumia bidhaa za ndani katika kutekeleza Mradi huo pia kununua bidhaa kutoka viwanda tofauti hapa nchini ili kuweka ushindani wa kibiashara pamoja na bei.
Kwa upande wa wenye viwanda, Dkt. Kalemani, aliwataka kuzalisha bidhaa zenye ubora na zenye viwango vinavyotakiwa ili kuendelea kukuza soko la ndani na nje pia kuuza bidhaa hizo kwa Bei nafuu zaidi.
Hata hivyo aliwaahidi wakandarasi hao kuwa kwa sasa Serikali itaharakisha ulipaji wa madeni wanayoidai tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wa TANESCO na REA, Dkt. Kalemani aliwataka kutimiza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani bado wananchi wengi wanahitaji kuunganishwa na huduma ya umeme hivyo waongeze juhudi na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.
Aliwataja wa Wahandisi walioteuliwa kusimamia Mradi wa REA III kuwa Ni
Mhandisi  Salum Inegeja  atakayesimamia Kanda ya Ziwa, Mhandisi John Kitonga Kanda ya Nyanda za Juu, Mhandisi Juma Mkobya Kanda ya Magharibi, na Mhandisi Ahmed Chinemba Kanda ya Kati.
Wengine ni Mhandisi Samuel Mgweno Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Christopher Bitesigirwe Kanda ya Pwani  pamoja na  Mhandisi Styden  Rwebangira Kanda ya Kusini.



Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiongea wakati uteuzi huo.

Washiriki wa mkutano wa wadau wanaotekeleza mradi wa REA III wakitoa maoni yao wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.

Washiriki wa mkutano wa wadau wanaotekeleza mradi wa REA III wakitoa maoni yao wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII
WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjccrqKHwUeSV7wXs6OjPd4dswZdq2PGY_0BLGylKTVHBDt8LAvWveRJJrBaRLt7XebxASovkuEW30x_XTXwqCVsujHITxodm4sy7wL65rDoSfnZOJCIfvk6y8q5n8Rx3krwukHEj3_PeI/s640/PICHA+15.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjccrqKHwUeSV7wXs6OjPd4dswZdq2PGY_0BLGylKTVHBDt8LAvWveRJJrBaRLt7XebxASovkuEW30x_XTXwqCVsujHITxodm4sy7wL65rDoSfnZOJCIfvk6y8q5n8Rx3krwukHEj3_PeI/s72-c/PICHA+15.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-dkt-ateuwa-kalemani-wahandisi-7.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-dkt-ateuwa-kalemani-wahandisi-7.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy