WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI LOLIONDO WALIPO IZUIA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALISILI NA UTALII
HomeJamii

WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI LOLIONDO WALIPO IZUIA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALISILI NA UTALII

Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardh...

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KIONGOZI MKUU WA JUMUIYA YA KIHINDU MWAMINARAYAN SANSTHA (BAPS) DUNIANI MTUKUFU MAHANT SWAMI MAHARAJ
TIB CORPRATE BANK YACHANGIA MILIONI 15.3 KWA MAENDELEO YA MKOA WA KATAVI
ENEO LA LEBANON SOKO LA SAMAKI LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM KINARA KWA UKATILI WA KIJINSIA

Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali halisi ya mgogoro uliopo.
Magari yaliyokuwa yamebeba wajumbe wa kamati hiyo yakiwa yameegeshwa baada ya wananchi kuzuia msafara huo wakishikiza kamati kusikiliza kero walizokuwa nazo.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wa kuzungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero zao.

Katika Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro  uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara

Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.

Wajumbe wa kamati ya Ardhi,Maliasili na Utalii waliozungumza na Clouds Tv ,Sebastian Kapufi na Dkt Godwin Mollel wamesema hatua ya wafugaji hao kuzuia msafara wa kamati ililenga kuvuruga ziara hiyo.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii wakiwemo wataalamu na wanasheria imewasili Loliondo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi,Atashasta Nditiye na kufanya ziara ya kutembelea eneo lenye ukubwa kilomita 1500 za mraba linalokusudiwa kurejeshwa katika hifadhi .

Eneo hili linatajwa kuwa na vyanzo vingi vya maji yanavyotiririka katika mto Gurumeti  unaopita katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti ambao ni muhimu kiikolojia kutokana na maji yake kutumiwa na wanyama pori katika hifadhi hiyo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI LOLIONDO WALIPO IZUIA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALISILI NA UTALII
WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI LOLIONDO WALIPO IZUIA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALISILI NA UTALII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0Su-DUb_FU_WbPMoq8QBLvT-hS5pBtg2VtLcsOOQiYy551OKMgzyxImYpGrDFe-qxp5Uomm30zX9gP2zcU94-FCK3VA_mywInEMMwoFMmXSjf8djpcK8R4A5oKhCg_fzeS-7KDZZbj6uR/s640/5Y2A0454.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0Su-DUb_FU_WbPMoq8QBLvT-hS5pBtg2VtLcsOOQiYy551OKMgzyxImYpGrDFe-qxp5Uomm30zX9gP2zcU94-FCK3VA_mywInEMMwoFMmXSjf8djpcK8R4A5oKhCg_fzeS-7KDZZbj6uR/s72-c/5Y2A0454.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wananchi-wa-jamii-ya-wafugaji-loliondo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wananchi-wa-jamii-ya-wafugaji-loliondo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy