Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na M...
Gaudence
Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya
kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa
kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.
Gaudence
Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka rekodi
baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu.
Lekule akifurahia mara baada ya kufanikiwa kuweka ekodi ya kutumia muda wa saa 8:36 kupanda Mlima Kilimajaro na kushuka.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MTANZANIA
,Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima kwa kasi
(Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na
Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina
nafasi kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.
Lekule
anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda kwa
muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36
alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi binafsi na za serikali kujitokeza
kudhamini wanamichezo kutokana na eneo hilo upo uwezekano wa kujitangaza
zaidi kidunia.
Akizungumza
na gazeti hili katika mahojiano maalum,Gaudence alisema kwa sasa yupo
katika maandalizi ya kuweka rekodi mpya katika milima mirefu na maarufu
Duniani kwa kufanya mazoezi ya awali hapa nchini na baadae nje ya nchi.
“
Nashukuru kuitangaza Tanzania kidunia na tayari nimepata mialiko mingi
ya kwenda nje kushiriki mashindano ya Mountain Run ,Lengo langu ni
kuweka rekodi katika milima mirefu duniani hivyo bado naendelea na
mazoezi na nitaendelea kufanya mazoezi hapa kwetu na badaae nje ya
Tanzania”alisema Gaudence .
Alisema
hadi sasa rekodi ya Dunia inashikiliwa na raia wa nchi ya Ecuador, Karl
Egloff aliyetumia muda wa saa 6:53 kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro
,rekodi aliyoweka mwaka 2014 akivunja rekodi ya Kilians Jornet raia
wa Hispania aliyetumia muda wa saa 7:20 kupanda na kushuka mlima
Kilimanjaro mwaka 2010.
Lekule
alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni mabadiliko hali ya hewa
inayochangia kushindwa kufanya mazoezi na upatikanaji wa mahitaji kama
chakula pamoja na mavazi kwa ajili ya mchezo huo unafanyika kuanzia
urefu wa mita 3500 hadi 5800.
Akizungumzia
kilichomsukuma kushiriki mcezo mchezo huo,Lekule ,mkazi wa kiraracha
Marangu wilaya ya Moshi alisema raia wa kigeni wamekuwa wakishiriki
katika michezo ya aina hiyo kwa ajili ya kuweka rekodi hivyo akaona ni
wakati wa waafrika pia kushiriki katika uwekaji wa rekodi Duniani.
Alisema
raia wa Ecuador ,anayeshikilia rekodi ya dunia aliposikia ameweka
rekodi akiwa ni mwafrika na Mtanzania wa Kwanza alituma salamu za
pongezi huku akimtaka kwenda kwenye milima iliyopo nchi za nje kutafuta
rekodi nyinine.
“
Egloff alifurahi sana na kunipa moyo na kunitaka nikatafute rekodi nje
ya Afrika kwa sababu nina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri Ulaya na kuipa
sifa Tanzania,ni ngumu sana mtu kukimbia kwenye urefu kama uliopo Mlima
Kilimanjaro na katika maisha inahitaji moyo sana.”alisema Lekule.
Rekodi za kidunia.
Mara
ya kwanza rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kasi kwa Afrika
ilikua inashikiliwa na Saimon Mtui akitumia muda wa saa 9 : 20 mwaka
2006, baadae raia wa Hspania Kilians Jornet alitumia muda wa saa
7:20 mwaka 2010.
COMMENTS