Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Ahmed Olotu (Mzee Chilo) mara baada ya kupokea shilingi laki sita na ishiri...
Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Ahmed Olotu (Mzee Chilo) mara
baada ya kupokea shilingi laki sita na ishirini kutoka kwa Mtandao wa
wasanii (SHIWATA) ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la
Ardhi Mkoani Kagera.Wengine pichani ni Mkurugenzi Idara ya uratibu Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Gen. Mbazi Msuya na Caasim Taalib (wa tano
kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyabiashara ndogondogo soko la kariakoo mara baada ya kupokea msaada
wa nguo mchanganyiko, midoli na kanzu wenye thamani ya shilingi milioni 2
ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani
Kagera.
……………………………………………………………….
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na
nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa wadau mbalimbali.
Makabidhiano
ya michango hiyo yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Nawashukuru
kwa kuamua kutumia siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha Baba wa Taifa
Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,”
amesema.
Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.
Misaada
hiyo imetolewa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sh. milioni 20,
Mtandao wa Wasanii Tanzania sh. 620,000 na nguo mifuko miwili, Chama cha
Makatibu Mahsusi (TAPSEA) sh. milioni tano.
Wengine
ni Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo soko la Kariakoo ambao wametoa
marobota mawili ya nguo (suruali, kanzu na nguo za akinamama na moja la
wanasesere kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa vyote vikiwa na
thamani ya sh. milioni mbili.
Fedha
na nguo hizo vimetolewa kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
Pia
tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081
zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku
wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali .
COMMENTS