Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa rasmi leo na Mwenyekiti w...
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa
rasmi leo na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mfalme Mswati III wa Swaziland
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe –Swaziland.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dakta John Pombe Magufuli
anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) watajadili mambo
mbalimbali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi wa Jumuiya hiyo hasa
katika sekta za viwanda, elimu, miundombinu, mtangamano wa masoko,
ulinzi na usalama pamoja na kuweka mfumo wa kushirikisha sekta binafsi
katika ngazi zote za utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwenye jumuiya
hiyo.
Akifungua
Mkutano mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa
Afrika Mfalme Mswati III wa Swaziland amezitaka nchi wanachama wa
jumuiya hiyo kuimarisha mipango na mikakati inayolenga kuhakikisha
wananchi wa nchi za jumuiya hiyo wanapata huduma bora za kijamii.
Mfalme
Mswati III amesema nchi wanachama wa SADC zikishirikiana kwa pamoja
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Jumuiya hiyo anaimani kuwa
tatizo la uhaba wa ajira na umaskini litapungua kwa kiasi kikubwa kwenye
nchi hizo.
Ameeleza
kuwa ili nchi wanachama wa SADC ziweze kuimarisha shughuli za uchumi ni
muhimu kwa mkakati wa kuendeleza na kujenga viwanda ukatiliwa mkazo kwa
sababu nchi hizo zina rasilimali nyingi ikiwemo madini, mifugo na
masuala ya utalii.
Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) watajadili mambo
mbalimbali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi wa Jumuiya hiyo hasa
katika sekta za viwanda, elimu, miundombinu, mtangamano wa masoko,
ulinzi na usalama pamoja na kuweka mfumo wa kushirikisha sekta binafsi
katika ngazi zote za utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwenye jumuiya
hiyo.
Kabla
ya kufanyika kwa mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya wataalamu,
Makatibu Makuu na Mawaziri wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ujumbe
wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri unaongozwa na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga akisaidiana
na Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Katika
ngazi ya Makatibu Wakuu ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Balozi Aziz
Mlima Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mbabane- Swaziland.
COMMENTS