Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimis...
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria
nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo
jijini Dar es Salaam.(PICHA NA BENJAMIN
SAWE- MAELEZO)
NA BENJAMIN SAWE MAELEZO.
RAIS John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye
kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa
mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2017, Kaimu Jaji Mkuu,
Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada
mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango
mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha
ukuaji wa uchumi.
Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi
maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja
Katika matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi
maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea
maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote
zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya
kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria
Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri
katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za
kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na
kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria
Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni
mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa
Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.
Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto)
akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku
ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama
vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria
nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo
jijini Dar es Salaam.
COMMENTS