Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kudhibioti na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga. (PICHA YA MAKTABA) NA K-VIS BLOG KAM...
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kudhibioti na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga. (PICHA YA MAKTABA)
NA K-VIS BLOG
KAMISHNA Mkuu wa
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Rogers Sianga, amesema
uchunguzi wao hadi sasa hawajaona uhusika wa moja kwa moja wa wanasiasa hapa
nchini kwenye biashara ya dawa za kulevya.
“Bahati nzuri
unaposhughulika na dawa za kulevya watu hawa hawajifichi, tabia zao, mienendo
yao na maisha yao hayajifichi, kwa kiasi kikubwa wanasiasa hatuoni connection ya uhusika wao, lakini siwezi
kusema kwamba hakuna watu wa aina hii wanaohusika, lakini huko tuendako,
yawezekana tukawajua hawa yawezekana atakayekamatwa ni jamaa yake, mtoto wake
au ndugu yake.
Akizungumza
asubuhi hii ya leo Jumapili Februari 19, 2017 na mtangazaji Tido Mhando kwenye
kipindi cha Funguka, Kamishna Mkuu
Sianga pia amesema Tanzania wapo Wafanyabiashara wakubwa kingpin wawili wa kuuza dawa za kulevya wanaotambulika kimataifa,
mmoja yuko gereza la Segerea alikamatwa tarehe 31/6/ 2010 ambaye ni mwanamama.
Mwana mama huyu
huko jimbo la Hanova nchini Ujerumani ana kesi 40 za watu aliowatuma kufanya
biashara hiyo ya dawa za kulevya.
Mtu wa pili ni
mwanaume yuko kwenye gereza moja hapa nchini, alitajwa kuwa ni mfanyabiashara
mkubwa wa dawa za kulevya, Marekani Ulaya, Afrika na Australia wamemtaja kuwa
wanamtafuta.
Huyu alikuwa na
nguvu ya kuagiza dawa za kulevya kwenye viwanda vinavyozalisha akielekeza
kiwango cha Purity ya dawa
anazohitaji, mathalan 7% ya kiwango cha level
ya purity ni Mtanzania.
Pia amezungumzia
suala la Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kupelekwa
mahakamani kwa kosa la kutumia dawa za kulevya.
“Watuamiaji wa
dawa za kulevya tunawakamata kama vyanzo vyetu vya habari, ili kujua ni wapi
wanapata hayo madawa, nay eye hatyumuachi, tunampeleka kwenye rehab ili apate
matibabu, kwa wale wanaokataa, tunamuweka kwa siku mbili tatu ili ile AROSTO
impate na hatimaye atataja tu.” Alisema.
Kwa wale ambao
wameshiriki vizuri, hatuwapeleki mahakamani, sisi tunachokifanya ni kumsaidia
ili kumuondoa kwenye uraibu”.
Hayo ameyasema,
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini,
Rogers Sianga, wakati akiongea na Mtangazaji Tido Mhando kwenye kipindi cha Funguka kinachopeperushwa na Televisheni
ya Azam Tv ya jijini Dar es Salaam.
Pia Kamishna
Sianga amesema, katika kipindi uchunguzi wao hadi hivi sasa, bado hawajaona
uhusika wa moja kwa moja wa wanasiasa katika biashara ya dawa za kulevya.
Kamishna Rogers
pia alisema, Mtanzania mwingine alikamatwa 2014 lakini hajatangazwa kama kingpin lakini ana nguvu kubwa na yuko
gerezani.
Pia wako wengine
kadhaa wakubwa wako kwenye magerezani mbalimbali ambao wametetemesha bara la la
Afrika, amesema Kamishna Sianga.
“Suala la
kufanya biashara ya madawa ya kulevya , muundo ule unaotumika kusafirisha dawa
hizo sio wa kudumu, ukiondoa vingozi wa juu uliowakamata, inaundwa nhingine na
hakuna kinachosimama na hakuna kinachodumu it’s
never permanent inanyumbuka kila wakati, kwa hivyo kazi yetu ni mpekecho
tunaendelea kupambana nao.
“Katika jambo lolote political will ni jambo
muhimu sana, inakusaidia wewe mtendaji kujijua je niko salama, hata ukiwa
unashughulika na hao vigogo unakuwa huna wasiwasi, unakuwa na ari ya kufanya
kazi.” Alisema.
“Sekeseke la
kupambana na dawa za kulevya linahitaji nguvu, diplomasia haina nafasi sana,
kinachobadilisha ni mbinu au taratibu za hatua tunazochukua, mapambano ni yale
yale, tumepokea orodha, kila jina tulilopewa tunakwenda nalo, watu hivi sasa
wako mtaani, tayari tunaye mtu mkubwa tu tumemkamata asubuhi ya leo, na
tunaanza kukusanya maelezo yake.
“Lakini
tunajaribu kuwa makini na taarifa tunazopata, kwani inawezekana mtu akataja
jina la mtu kwa chuki, na hivyo tukajikuta tunaingia kwenye matatizo makubwa.” Alisema.
Tunatumia neon “JAPAN”
katika kufanyabkazi zetu, neon hili Japan halimaanishi nchi ya Ujapan, la
hasha, hili neon linatumika katika shughuli zetu hizi na maana yake ni hii J
ni-, Justify, (Sababu), Authority (Mamlaka kisheria), Proportional (nguvu unayotumia),
Admini (Utawala), Necessity (Umuhimu).
COMMENTS