THBUB YALAANI OFISI ZA WANASHERIA KULIPULIWA KWA BOMU
HomeJamii

THBUB YALAANI OFISI ZA WANASHERIA KULIPULIWA KWA BOMU

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 213...

SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI
HAMASA INAHITAJIKA KWA WASICHANA WANAOPENDA KUJIFUNZA TEHAMA NCHINI
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI


-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz

Agosti 28, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

THBUB yalaani ofisi za Wanasheria kulipuliwa kwa bomu

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inapenda kutoa tamko la kulaani kitendo cha kupigwa bomu ofisi za wanasheria wa IMMMA zilizoko barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 26 Agosti, 2017.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na kitendo hicho ambacho kinaashiria uhalifu wenye nia ya kutisha wanasheria wasitekeleze majukumu yao ya kisheria ya kutetea wateja wao.

Tume inasisitiza kuwa dhana ya utawala bora inategemea utawala wa sheria, ambao utaathirika iwapo wanasheria watatishwa na matukio kama ya kupigwa mabomu au vitendo vinginevyo vitakavyowanyima uhuru wa kufanya kazi zao.

Tume inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria.

Aidha, Tume inautaka uongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kusitisha tangazo lao la kuwataka Mawakili kususia vikao vya Mahakama na Mabaraza kwa siku mbili kwani mgomo huo hautakuwa na maana kwa vile vyombo vya usalama vimeishaanza kufanya uchunguzi. Pia ni vyema TLS ikasitisha mgomo huo kwani utawaathiri zaidi wateja wao ambao hawahusiki na tukio la kupiga bomu.

Imetolewa na:
(SIGNED)

Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Agosti 28, 2017

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: THBUB YALAANI OFISI ZA WANASHERIA KULIPULIWA KWA BOMU
THBUB YALAANI OFISI ZA WANASHERIA KULIPULIWA KWA BOMU
https://lh6.googleusercontent.com/16NXspSG6YI6jordV7myJ0S51fDfqH2QeIcEB3qk9jeJv_V7Wf5BoWUmBy7KCrb54vxUSGHm1JkC5m8cuZduoMzVG0hQZPmMoPr4X5dvpa64pld0yZAbEh1iaCrjGRbSUSFT_w54I5ne5QkybQ
https://lh6.googleusercontent.com/16NXspSG6YI6jordV7myJ0S51fDfqH2QeIcEB3qk9jeJv_V7Wf5BoWUmBy7KCrb54vxUSGHm1JkC5m8cuZduoMzVG0hQZPmMoPr4X5dvpa64pld0yZAbEh1iaCrjGRbSUSFT_w54I5ne5QkybQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/thbub-yalaani-ofisi-za-wanasheria.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/thbub-yalaani-ofisi-za-wanasheria.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy