Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ch...
- Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari 2017 linalofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua moja ya semina za mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
KILA ifikapo
Mei 3 ya kila mwaka wanahabari na wadau wa vyombo vya habari
ulimwenguni huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Maadhimisho ya mwaka huu (2017) kitaifa nchini Tanzania yalifanyika
mkoani Mwanza na kushirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa
vyombo vya habari.
Miongoni
mwa hoja zilizoteka mijadala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2017 jijini Mwanza ni suala zima la
usalama wa wanahabari wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao pamoja na uwepo
wa mafunzo anuai ya mara kwa mara kwa wanahabari kuwanoa zaidi.
Chama
cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), ni miongoni mwa taasisi wadau
waliofanikisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani mwaka 2017 kitaifa yaliofanyika mkoani Mwanza. Bi. Valerie Msoka
ni Mwanachama wa TAMWA, akizungumza katika maadhimisho ya mwaka huu
kuwasilisha ujumbe wa chama hicho kwa wadau wa habari.
Anasema
TAMWA imejitahidi katika kuwanoa wanahabari ili kuhakikisha wanabobea
kwenye maeneo mbalimbali ya uandishi wa habari huku lengo likiwa
kuwajengea uwezo zaidi. Bi. Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA hapo nyuma kabla ya uongoziwa wa Mkurugenzi wa sasa wa
chama hicho, Edda Sanga anabainisha wamekuwa mstari wa mbele katika
kuchangia weledi na ubobezi wa wanahabari hasa katika uandishi wa habari
za ukatili kwa jamii.
Anasema
tamwa katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kwa kipindi
cha mwaka 2015 na 2016 imeelimisha idadi kubwa ya wanahabari kwenye
ubobezi wa uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia eneo ambalo
limekuwa likionekana kupwaya kiuandishi.
Wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2350 na
wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsia ya kuandika habari za ukatili
wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo
hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali.
Anasema
waandishi hao baada ya kupata mafunzo hayo wamekuwa wakitumia ujuzi huo
kuandika na kuibua habari za vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo
ambalo limesaidia baadhi ya maeneo mamlaka husika kuchukua hatua juu ya
vitendo hivyo, hali ambayo imekuwa ikisaidia kupungua kiasi fulani kwa
vitendo hivyo kwenye jamii ukilinganisha na hapo awali.
- Baadhi ya wanahabari wapiga picha ambao walishiriki mafunzo ya upigaji picha za ukatili yaliyoandaliwa na TAMWA wakimsikiliza mkufunzi wa mafunzo hayo, Mwanzo L. Millinga (wa kwanza kulia) kutoka ‘Practical School of Journalism’ (PSJ).
- Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kulia) akizungumza katika moja ya mikutano ya mafunzo kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa TAMWA.
Aidha
Bi. Msoka anaongeza kuwa utaratibu huo wa kuwajengea uwezo wanahabari
umekuwa ukifanywa mikoa mbalimbali huku ukijumuisha wanahabari
kuandaliwa kimafunzo katika semina kadhaa na baadaye kufuatiliwa kwenye
utendaji ili kubaini mabadiliko kimafanikio kabla ya mafunzo na baada ya
mafunzo waliyopata. Wananchi kwa upande mmoja nao wamekuwa wakihamasika
na kutumia vyombo vya habari katika kuibua matukio hayo ya kikatili,
jambo ambalo limeanza kuleta mafanikio kiasi fulani.
Bi.
Msoka anaendelea kubainisha kuwa TAMWA katika kutekeleza mradi wake wa
GEWE II kimeweza kuunda kamati za kuelimisha jamii jinsi ya
kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya kumi za
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, ambazo zinawahusisha wanahabari ili
kuwezesha jamii kushirikiana na vyombo vya habari kuweza kuvitolea
taarifa vitendo hivyo bila woga. Anaeleza kuwa kwa kisi kikubwa kamati
hizo zimesaidia kuibua matukio hayo kwa kiasi kikubwa kwa vyombo vya
habari.
Pamoja
na hayo Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kinaamini kuwa kupitia
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ya mwaka huu
(2017) wanahabari kwa kutumia changamoto zilizoibuka dhidi yao, katika
kujitathmini, watafanya kazi zao kwa weledi na uaminifu ikiwa ni pamoja
habari zenye usawa wa pande zote husika. Hii ni pamoja kujitahidi
wanatasnia hiyo kuibua mambo yanayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo
ili yafanyiwe kazi, pia kujiepusha na habari ambazo kwa sehemu zinaweza
kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao wenyewe au wananchi katika
taifa la Tanzania.
Kama
hiyo haitoshi TAMWA, imeendelea kuwanoa wanahabari katika nyanja
nyingine za kimafunzo. TAMWA ilijiunga katika mapambano ya ajali za
barabarani kwa kutoa mafunzo kwa wanahabari mbalimbali. Katika ufafanuzi
juu ya hatua hiyo inabainisha kuwa ajali za barabarani zimekuwa
zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga anasema katika moja ya mafunzo kwa
wanahbari kuwa wana kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali
nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi
kikubwa. Anasema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na
kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto
pasipo na msaada kwa kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika
familia.
- Sehemu ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam.
- Sehemu ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam.
COMMENTS