KAIMU MD WA TANESCO, DKT MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO
HomeJamii

KAIMU MD WA TANESCO, DKT MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito Mwinuka (pich...

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI
UZINDUZI WA iSwapMyBookS.COM WASAIDIA KUHAMASISHA USOMAJI WA VITABU NCHINI TANZANIA
RAIS MAGUFULI AIPONGEZA PSPF KWA KUBUNI MAFUNZO YA KUWATAYARISHA WASTAAFU WATARAJIWA






NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito Mwinuka (pichani kulia), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na
kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt. Mwinuka alisema,  ongezeko la watu na
shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na
ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo
vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.
“Barabra zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za
kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi
kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo
vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa
Kilovolti 132.
Dkt. Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa
Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.


 Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
 Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika.
 Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito E.Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini vilivyoko Wilayani Temeka. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
 Dkt. Mwinuka (mbele), baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Mwinuka, (wapili kulia) akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere, (kushoto), wakati alipotembelea kituo cha Kurasini. Kulia ni
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.

 Muhandisi mwandamizi wa miradi wa TANESCO, Mhandisi Rosmystice Luteganya (kushoto), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka, kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Mwinuka, (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo.
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya, (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, kwenye chuo cha TANESCO jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Dkt. Mwinuka, Mhandisi Chegere na Mhandisi Mashalo.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Jengo la kituo cha bkupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovolti 132 cha Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limekamilika.
Meneja wa TANESCO Wilayani Temeke, Mhandisi, Jahulula Maendeleo (kulia), akizungumza na maafisa wa TANESCO wakati wakimsibiri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Rito E. Mwinuka kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAIMU MD WA TANESCO, DKT MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO
KAIMU MD WA TANESCO, DKT MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg38lNqbmH6qEoj07fNft7xrUEaSt7drN8fKbQC0oNmciQM3Fuqh9IgkRCmjvnNKlkB73PfrzkcJ_sM3CVTp6wR2EAwm0OmlpT4VXW55Y3pJ2vmACKnLjGew2CsNI4jIS2nhcQb7zguHYk/s640/5R5A3705.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg38lNqbmH6qEoj07fNft7xrUEaSt7drN8fKbQC0oNmciQM3Fuqh9IgkRCmjvnNKlkB73PfrzkcJ_sM3CVTp6wR2EAwm0OmlpT4VXW55Y3pJ2vmACKnLjGew2CsNI4jIS2nhcQb7zguHYk/s72-c/5R5A3705.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/kaimu-md-wa-tanesco-dkt-mwinuka-akagua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/kaimu-md-wa-tanesco-dkt-mwinuka-akagua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy