KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI
HomeJamii

KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya...

HOSPITALI YA AGA KHAN YAANZA KUTOA BURE HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WA MATITI KWA AKINA MAMA
WAZIRI MKUU AWASILI TOKEA NCHINI CANADA
VIJANA WAJADILI MASWALA YA UCHUMI, DEMOKRASIA NA MAENDELEO KITAIFA DAR ES SALAAM


 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.

 Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na 
wajumbe wa kamati hiyo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi  wa Bunju B
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.

Na Dotto Mwaibale

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuchangamkia nyumba zinazojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), ili kupata makazi bora baada ya kustaafu.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Josephat Asunga wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba inayofanywa na TBA jijini Dar es Salaam jana.

"Nawaomba watumishi wa umma kuzichangamkia nyumba hizi ambazo kwa  wao wanafursa ya kukopeshwa na kulipa deni polepole" alisema Asunga.

Alisema nyumba hizo zimejengwa na kuwekewa miundombinu mizuri hivyo kuwa ni sehemu bora ya kuishi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga alisema nyumba zinazojengwa na TBA bei yake ni ndogo ukilinganisha na zile zinazojengwa na watu wengine.

"Hapa kwetu bei ya nyumba inaanzia sh.milioni 35 hadi milioni 200 wakati  maeneo mengine ni kuanzia sh.milioni 600" alisema Mwakalinga.

Alisema ujenzi wa nyumba hizo unakwenda sanjari na miundombinu yake na mahitaji mengine kama soko, bustani na  maegesho ya magari.

Alisema katika awamu ya tatu ya mradi TBA walipata mkopo wa sh.Bilioni 25 ambapo hadi Februari 2017 walipata mkopo wa sh.Bilioni 19.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia watumishi wa umma.

Alisema katika awamu ya pili ya mradi huo jumla ya nyumba 160 za aina tofauti zinaendelea kujengwa za zipo katika hatua mbalimbali, ambapo nyumba 64 zipo kwenye hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa na nyumba 96 bado zipo kwenye hatua ya msingi na zilitarajiwa kujengwa kwa kutumia mfumo wa "Lunnel Forwork System"

Akizungumzia changamoto katika mradi huo alisema watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja ndani ya eneo la mradi hivyo kupunguza idadi ya nyumba zilizokusudiwa kujengwa katika hatua za awali za awamu ya tatu ya mradi.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni kupatikana kwa malighafi mbalimbali za ujenzi hasa mawe, nondo hivyo kupunguza kasi ya ujenzi, upungufu wa fedha za utekelezaji wa mradi, kupanda kwa gharama za ujenzi kutokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

Alisema ili kupunguza gharama za kununua vifaa vya ujenzi  wakala amekuwa akienda kuvinunua moja kwa moja kiwandani.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI
KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSWQzU-Pjrz7czPoEHJfv2xz46Qi3GoYsMeg7ds_FkkWLNcapdx-bB12A3y7jmWBqfeOFFpJVHRUnDzDjc6Zo-9QQNmWr0_9U1toYcek9fzGewcQSLkrCWP4xYujrorWPb54x904P9qBl3/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSWQzU-Pjrz7czPoEHJfv2xz46Qi3GoYsMeg7ds_FkkWLNcapdx-bB12A3y7jmWBqfeOFFpJVHRUnDzDjc6Zo-9QQNmWr0_9U1toYcek9fzGewcQSLkrCWP4xYujrorWPb54x904P9qBl3/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/kamati-ya-bunge-yawataka-watumishi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/kamati-ya-bunge-yawataka-watumishi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy