Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua ...
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa
Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania).
Uzinduzi huo umefanyika June 2 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba
Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi
na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi Atashasta Nditiye
(kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel
Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi,
Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia
Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu
wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu
(hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
Sehemu
ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake
nchini pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi
Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu
maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mpango wa
Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania).
Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni
(katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa
serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa
yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia
Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo
umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam.
(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
COMMENTS