WANANCHI WAOMBA ENEO LAO KUPIMWA NA KUGAWIWA VIWANJA NJOMBE
HomeMikoani

WANANCHI WAOMBA ENEO LAO KUPIMWA NA KUGAWIWA VIWANJA NJOMBE

  Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadha...

MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA NYUMBANI, WAAJIRI PAMOJA NA WATENDAJI JIJINI MWANZA
DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA
NAIBU WAZIRI AWESO AWATAKA WAKAZI WA PANGANI KUWA NA MSHIKAMANO ILI KUPATA MAENDELEO
























 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara





Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao.



WANANCHI halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa tena viwanja.


Wananchi wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.

Nestori Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.

Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.


Afisa ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka 2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.

Alisema kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.

Katika hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa amani bila bughuza.


Hata hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.

Alisema kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.


Hata hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi kushindwa kuvimiliki.


Na Furaha Eliabu wa Habari Online na Elimtaa


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WAOMBA ENEO LAO KUPIMWA NA KUGAWIWA VIWANJA NJOMBE
WANANCHI WAOMBA ENEO LAO KUPIMWA NA KUGAWIWA VIWANJA NJOMBE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvq2mRtNi600_yvE3wrkKKXWhTGEGXcckal2XM0bL-1PTVpGscDBsuISLfo-uryDZJUtJVbxA4j1mJ_rLR_c_6GLXRTAYvhMp8waoJv2qacUwJ5VSKcMdr1DmysV-oS53X7i5bNOa7Vcg/s640/DSC_1167.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvq2mRtNi600_yvE3wrkKKXWhTGEGXcckal2XM0bL-1PTVpGscDBsuISLfo-uryDZJUtJVbxA4j1mJ_rLR_c_6GLXRTAYvhMp8waoJv2qacUwJ5VSKcMdr1DmysV-oS53X7i5bNOa7Vcg/s72-c/DSC_1167.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wananchi-waomba-eneo-lao-kupimwa-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wananchi-waomba-eneo-lao-kupimwa-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy