WAMACHINGA DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWARUHUSU KUFANYA BIASHARA BILA KUBUGUDHIWA
HomeJamii

WAMACHINGA DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWARUHUSU KUFANYA BIASHARA BILA KUBUGUDHIWA

  Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika  Kamtanda Hamisi akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi  wakati akitoa maoni yake baa...









 Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika 
Kamtanda Hamisi akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi 
wakati akitoa maoni yake baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa. Habari na maelezo ya wafanyabiashara wengine soma habari hapo chini.

 Muuza mitumba Hassan Bakar.

 Mfanyabiashara Juma Abdul.

 
 Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo.

 Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan.

Mfanyabiashara wa mitumba Salum Mwinyimkuu.

Wauza mitumba katika Soko la Tandika wakiwa wamepozi kwa furaha baada ya Rais Dk. John Magufuli kuwaruhusu kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa.


Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanyabiashara zao bila ya kubugudhiwa na kumtaja kuwa ni kiongozi wa wanyonge na watu wa chini.

Kauli hiyo wameitoa leo asubuhi wakati wakitoa maoni yao baada ya Rais kutoa tamko hilo Dar es Salaam jana.

Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika Kamtanda Hamisi alimshukuru rais kwa kuwaruhusu na kuwajali watu wa chini.

"Nawaomba wafanyabiashara wenzangu ruhusa ya rais isiwe kibali cha sisi kuanza kupanga biashara zetu barabarani tufuate sheria" alisema Hamisi.

Muuza mitumba Hassan Bakar alisema Rais Magufuli yupo vizuri tunakila sababu ya kumpongeza katika jambo hilo la kuwatetea wanyonge yupo katika mstari ulionyooka na tumeteseka kwa miaka mingi.

Juma Abdul alisema anafuraha kwa uamuzi huo wa rais kwani ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa uchaguzi mkuu.

"Tulitukanwa sana na kunyang'anywa bidhaa zetu sasa baba yetu Magufuli ametuona na kutuondoa kwenye mateso hayo" alisema Abdul.

Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo alisema walikuwa wakiishi kama digidigi na kupoteza bidhaa zao baada ya kuchukuliwa na mgambo sasa vitendo hivyo vimekoma kupitia kwa rais wetu tunampongeza kwa hatua hiyo.

Salum Mwinyimkuu alisema Rais yupo sahihi kwa hatua hiyo,  kazi hii tunayoifanya ndio ajira yetu inayotuwezesha kuishi na familia zetu.

Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan alisema wanamshukuru rais kwa ruhusa hiyo hivyo akatoa mwito kwa wenzake kuzingatia sheria ya kutofanya biashara barabarani na kuzuia vyombo vya moto visipite. 


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAMACHINGA DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWARUHUSU KUFANYA BIASHARA BILA KUBUGUDHIWA
WAMACHINGA DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWARUHUSU KUFANYA BIASHARA BILA KUBUGUDHIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5yatNlXko6g2l2REudqrVqvcQPzsTJ0bRkcn4O15c1IGL6r097zsBVnUOgldrb2lURHIhRUOcigkdTY5N_o50FNykkplRYyCd9tAOWlZ3v7gAioIl2fDuZYSLjqbSwG82xhn-mjBeiNkz/s640/IMG_5123.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5yatNlXko6g2l2REudqrVqvcQPzsTJ0bRkcn4O15c1IGL6r097zsBVnUOgldrb2lURHIhRUOcigkdTY5N_o50FNykkplRYyCd9tAOWlZ3v7gAioIl2fDuZYSLjqbSwG82xhn-mjBeiNkz/s72-c/IMG_5123.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wamachinga-dar-es-salaam-wampongeza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wamachinga-dar-es-salaam-wampongeza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy