WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA KUILINDA AMANI
Mhe. Kassim Majaliwa
HomeJamii

WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA KUILINDA AMANI

*Asisitiza mapambano dhidi ya viashiria vya uvunjifu wa amani WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walip...

SERIKALI KUANGALIA UPYA KANUNI ZA TAFITI ILI ZIWEZE KUFANYA KAZI KWA WAKATI
WAZIRI UMMY ATEMBELEA KITUO CHA AFYA BUGURUNI
HABARI KUHUSU ZIARA AYA RAIS WA UTURUKI


*Asisitiza mapambano dhidi ya viashiria vya uvunjifu wa amani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.



Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 31, 2018) kwenye Mkutano Mkuu wa BAKWATA uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo.

“Dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa katika amani ya nchi yetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu”

Waziri Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa sana kwa binadamu na ndio maana wote wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au kikundi chochote kujaribu kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea kuwaunganisha waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao au madhehebu yao.

Waziri Mkuu amesema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote amekuwa akisisitiza jambo hilo na kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo chao.

“Ni muhimu sana kwa ninyi wasaidizi wa Mufti mlio kusanyika hapa muhakikishe mnalisimamia hili katika maeneo yenu. Katika hili napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yenu iko pamoja Mheshimiwa Mufti kutekeleza nia hiyo njema.”

Amesema ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ni kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kusikiliza maoni, ushauri na  mapendekezo yeyote kutoka kwa viongozi wa dini . ‘Milango iko wazi saa zote ‘

Ameongeza kuwa yeye si mtaalamu sana kama walivyo Masheikh hao lakini anakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani sura Al Imran aya ya 103 yanayosema “ Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane”

Mkutano huo umehudhuriwa na  Sheikh Mkuu wa Mufti wa Tanzania Sheikh Zubeir, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wajumbe wa Baraza la Ulamaa, Masheikh na viongozi wa BAKWATA wa mikoa na wilaya zote Tanzania.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MACHI 31, 2018.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA KUILINDA AMANI
WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA KUILINDA AMANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgonxoIBNlaSSb4fEV6KRxb6BLZrFZBmaaZSoNExCjWfdrXXJgKvvIaWwfu1baMblEpKu9bT8ZyA3tTSW4_0S5c_jnq_800xy9e16BNF_UZZcO_1IO_uKVDq5cm9pCxcGxrqtW2TY_kF1Y/s400/Mhe+Kassim+Majaliwa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgonxoIBNlaSSb4fEV6KRxb6BLZrFZBmaaZSoNExCjWfdrXXJgKvvIaWwfu1baMblEpKu9bT8ZyA3tTSW4_0S5c_jnq_800xy9e16BNF_UZZcO_1IO_uKVDq5cm9pCxcGxrqtW2TY_kF1Y/s72-c/Mhe+Kassim+Majaliwa.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-awaomba-viongozi-wa-dini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-awaomba-viongozi-wa-dini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy