Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasalimie wabunge wakati wa utambulisho wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. P...
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasalimie wabunge wakati wa utambulisho wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma (kushoto) wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo Mei 25, 2018.

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Mussa Zungu akiongoza kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa zao la korosho linaendea kuwanufaisha wakulima Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe. Mboni Mhita wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akitolea ufafanuzi tofauti iliyopo kati ya shule za Serikali na Binafsi na kusisitiza kwamba mitaala ya kimataifa imeruhusiwa ili kukidhi mahitaji ya raia wa kigeni wanaoishi nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Mbunge wa Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma.
COMMENTS