WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSAIDIZI WA PEMBEJEO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mawakala wa Pembejeo nchini, kwenye makazi yake eneo la Kilimani mjini Dodoma Aprili 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
HomeJamii

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSAIDIZI WA PEMBEJEO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Shenal Ny...

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WA NISHATI NA MADINI PROFESA NTALIKWA
JWTZ KUANZA KULIPA DENI WANALODAIWA NA TANESCO
WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA






WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Shenal Nyoni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kwa kuongeza gharama za pembejeo kwa kushirikiana na baadhi ya mawakala wa pembejeo za kilimo.

Amesema Serikali italipa madeni yote ya mawakala wa pembejeo za kilimo mara baada ya kukamilisha uhakiki na kujiridhisha juu ya uhalali wake, sababu bado inawahitaji mawakala ili kushirikiana nao katika kuhudumia wakulima kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Aprili 10, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kati yake na mawakala wa pembejeo za kilimo pamona na Maofisa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Gharama ya madeni ni kubwa kuliko pembejeo zilizosambazwa. Hii inatokana na udanganyifu mkubwa unaofanywa na mawakala kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali wanaohusika na masuala ya pembejeo,”

Amesema kuwa kwenye eneo la pembejeo kuna matatizo makubwa kutokana na baadhi ya Maofisa kuzungumza na mawakala na kuongeza gharama za pembejeo kwa lengo la kuibia Serikali na kisha kugawana fedha. “Sasa Serikali haiwezi kulipa madeni ya kutengenezwa bali tutawalipa stahili zenu baada ya uhakiki kukamilika kama nilivyosema awali,”.

Waziri Mkuu ameongeza mawakala wa pembejeo waliwasilisha Serikali deni la sh. bilioni 65.4 kwa huduma waliyoitoa katika mikoa 25 ambapo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekamilisha uhakiki wa madeni hayo kwa mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha ambayo madeni yake ni asilimia 70 ya madeni yote.

Amesema ripoti ya uhakiki wa mikoa nane kati ya 10 imetoka (imebaki Katavi na Kigoma) na kubainisha kuwa mikoa hiyo inadai sh. bilioni 36 kati ya hizo sh. bilioni 11 bado zinaendelea kuhakikiwa, sh. bilioni 14 zimekataliwa hivyo siyo madeni halali, sh. bilioni 8.2 ndiyo deni halali na sh. bilioni 2.3 zinachungizwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Waziri Mkuu amesema uhakiki wa madeni kwa mikoa 15 iliyobakia ambayo madeni yake ni asilimia 30 unaendelea ambapo amewasihi mawakala hao kuwa wavumilivu katika kipindi ambacho Serikali inafanya uhakiki kwa kuwa inataka itende haki kwa kila mtu kulipwa deni lake kwa kiwango kinachostahili na watakaobainika kufanya udanganyifu watachukuliwa hatua za kisheria.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P 980, DODOMA
JUMATATU, APRILI 10, 2017.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba baada ya kuzungumza na Mawakala wa Pembejeo nchini kwenye makazi yake eneo la Kilimani mjini Dodoma, Aprili 10, 2017.


Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akizungumza (kulia) na baadhi ya Mawakala wa Pembejeo nchini baada ya mazungumzo yao na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, eneo la Kilimani mjini Dodoma Aprili 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSAIDIZI WA PEMBEJEO
WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSAIDIZI WA PEMBEJEO
https://i.ytimg.com/vi/LX7cC2WDllo/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/LX7cC2WDllo/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/waziri-mkuu-amsimamisha-kazi-mkurugenzi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/waziri-mkuu-amsimamisha-kazi-mkurugenzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy