WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA
HomeJamii

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akioneshwa taarifa ya mapato na Meneja wa Kampuni ya Simu Nchin...

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF
MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA NSSF JIJINI ARUSHA, SERIKALI YAPUNGUZA DENI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
eGA KUIPUNGUZIA SERIKALI GHARAMA YA MAWASILIANO KWA NJIA YA SIMU

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akioneshwa taarifa ya mapato na Meneja wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, Bw. Salum Mbaya, wakati alipotembelea ofisini hapo leo.


Fundi Mitambo kutoka Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), Eng. Godfrey Mbise, akimpa maelezo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu mfumo wa utoaji huduma katika mkongo wa taifa mkoani humo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa uongozi wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, leo, mara baada ya kukagua mitambo na mifumo iliyopo ofisini hapo. 



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akishuka katika ndege ya Kampuni ya Ndege Nchini (ATCL), katika uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo. 



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), mkoa wa Kagera Bi. Dorice Uhagile, wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba ambapo amekagua uwanja huo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazokabili uwanja huo.

Meneja wa Shirika la Posta Nchini, mkoa wa Kagera Bi. Mary Nsangila, akitoa taarifa ya utendaji kazi wa shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua maendeleo ya Shirika hilo mkoani humo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia mbele) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), mkoa wa Kagera Eng. Zephrine Bahyona (wa pili kushoto mbele), wakati alipokuwa akikagua karakana yao na kuona changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………..

TTCL KUZALISHA DOLA MIL 50.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi miwili Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kuhakikisha kuwa inapata Dola za Kimarekani milioni 50 ili kuongeza pato kwa Kampuni na Taifa kwa ujumla kupitia Mkongo wa Taifa.

Akitoa agizo hilo leo, wilayani Bukoba mkoani Kagera, Waziri Prof. Mbarawa amesema agizo hilo limetokana na Serikali kuongeza masafa kwa kampuni hiyo kutoka 10 hadi 200 (MHZ) ambayo yana uwezo wa kuunganisha wateja wengi na wakubwa zaidi.

Amesisitiza makampuni ya Simu nchini kuchangamkia fursa ili kupata masafa yenye uwezo mkubwa kupitia mkongo huo.

“Hakikisheni mnajipanga kuipata hiyo fedha ndani ya miezi miwili na kuwapatia masafa ya kutosha wateja mlionao ndani na nje ya nchi na kujitahidi kuongeza wateja wengi zaidi”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, ameitaka TTCL kusogeza wigo wa kuwasiliana na wateja wakubwa ili kuwashawishi kununua masafa hayo kulingana na mahitaji yao na hivyo kutanua wigo wa kibiashara na kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa TTCL mkoa wa Kagera Bw. Salum Mbaya amemhakikishia Waziri huyo kuwa wataanza mara moja kazi ya kutembelea wateja wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwapatia taarifa za ongezeko la uwezo wa mkongo na kuwashiwishi kujiunga ili kupatiwa masafa wanayohitaji.

Bw. Mbaya ametaja kuwa mpaka kufikia sasa nchi zilizounganishwa na mkongo wa Taifa ni Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Kenya na Malawi.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea uwanja wa ndege wa Bukoba na kuahidi kutatua changamoto zinazoukabili uwanja wa ndege wa Bukoba ikiwemo kujenga jengo la kuongezea ndege (Control Tower) ili kuongeza ufanisi na usalama katika usafiri wa anga.

Naye, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini mkoa wa Kagera, Bi. Dorice Uhagile, licha ya kuelezea mafanikio mbalimbali kama vile ongezeko la ndege na wateja uwanjani hapo pia amefafanua changamoto mbalimbali zinazoukabili uwanja huo na kuiomba serikali iweze kuwatatulia.

Waziri Mbarawa ameanza ziara ya kikazi wilayani Bukoba, mkoani Kagera ambapo ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara yake
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA
WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVtsnipmQrqJtvmich9hPhafJf1Dws2nEwwyQOtR8MJ7OVHkGgtbqGGp5Yvw4lAGymHCahOX79QJc5jQiQAFNXNJjCQtkqmQLIYfJZOqNEUrz2PzbIcM7JUV4ysC4CAdTdwHpNL_Dcpr0/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVtsnipmQrqJtvmich9hPhafJf1Dws2nEwwyQOtR8MJ7OVHkGgtbqGGp5Yvw4lAGymHCahOX79QJc5jQiQAFNXNJjCQtkqmQLIYfJZOqNEUrz2PzbIcM7JUV4ysC4CAdTdwHpNL_Dcpr0/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mbarawa-akagua-miundombinu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mbarawa-akagua-miundombinu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy