MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha...

USALAMA MAHALA PA KAZI, TANESCO YAIBUKA KIDEDEA YAKABIDHIWA NGAO
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI
HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH) KUPANDIKIZA FIGO WAGONJWA 200 KWA MWAKA




Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.


Picha ya pamoja.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.


Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA). Makamu wa Rais alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”.


Kwa miaka mingi mmeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola, alisema Makamu wa Rais.


Aidha, mkutano huo uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli. “Naamini kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza Makamu wa Rais.


Pia Makamu wa Rais alisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sheria. Aliwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.


Mwisho Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa kuhakikisha inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa.


Imetolewa na :-


Ofisi ya Makamu wa Rais
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUFlclsmrtF8CyYNeBImWl3Ep-LCvrhwb6cNY2xTA7iEQEix0FLPmIAUurhDfOxArtv9-1AC84PRGyT4k-Nw3rlE-FtE9cmNifW7ScJ3LDRT9jBvHMIpsZN_EqWtqNucSXg_ee_biC6LBE/s640/8.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUFlclsmrtF8CyYNeBImWl3Ep-LCvrhwb6cNY2xTA7iEQEix0FLPmIAUurhDfOxArtv9-1AC84PRGyT4k-Nw3rlE-FtE9cmNifW7ScJ3LDRT9jBvHMIpsZN_EqWtqNucSXg_ee_biC6LBE/s72-c/8.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-siku.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-siku.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy