Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilikagua eneo liliopo Mtofaani kwenye Makutano ya Bara bara za...
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilikagua eneo
liliopo Mtofaani kwenye Makutano ya Bara bara za Hawaii na Masingi
ambalo liliombwa na Wananchi kwa shughuli za Kijamii lakini kwa sasa
kuna tetezi ya kumilikiwa na Mtu mwengine.
Balozi
Seif akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tawi la Mofaani Bwana
Iddi Sultan kuhusiana na utata wa eneo hilo linalomilikiwa na mtu
binafsi hivi sasa.
Balozi
Seif kushoto akiwa nyuma ya Ukuta wa Matofali uliojengwa kati kati ya
eneo hilo akijaribu kuangalia upande wa Pili wa eneo hilo lenye utata wa
umiliki. Aliyepo upande wa Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Mheshimiwa Hassan Khamis Hafid.
Eneo
la wazi liliopo Makutano ya Bara bara ya kuelekea Msingini na Hawaii
liliopo Mashariki mwa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Sehemu hilo.
Ukuta
wa matofali uliojengwa kati kati ya Eneo la wazi liliopo Makutano ya
Bara bara ya kuelekea Msingini na Hawaii lenye kuleta utata wa umiliki
wake. (Picha na – OMPR – ZNZ).
Wananchi
wa Shehia ya Mtofaani Masingini ndani ya Jimbo la Welezo wameiomba
Serikali Kuu kufikiria maombi yao ya kutaka kupewa eneo lililokuwa
likimilikiwa na Kikosi cha Kuzuia Magendo { KMKM } kwa ajili ya
kulitumia kwa shughuli zao za Kijamii.
Wamesema
eneo hilo ni sehemu pekee iliyowazi kwa shughuli za Kijamii katika
shehia ya Mtofaani ambalo linaweza kuwasaidia kwa ujenzi wa Soko,huduma
za Afya, Skuli na Michezo ili kuwaondoshea usumbufu Watoto na Wananchi
kufuata huduma hizo katika Masafa marefu.
Wananchi
hao walipaza sauti zao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua eneo hilo baada ya kupokea kilio
chao wanacholalamikia eneo hilo kumilikiwa na Mtu aliyetambulika kwa
jina Moja tu la Zahor ambae kwa sasa ameshaamua kulizunguushia Ukuta
eneo lote.
Walieleza
kwamba muda mrefu uliopita Kamati ya Maendeleo ya Eneo hilo kupitia
Sheha wa Shehia hiyo iliwahi kupeleka maombi yao ili kupatia eneo hilo
lakini jitihada hizo hazikufanikiwa na badala yake kushuhudia ugawaji wa
Viwanja uliopelekea kuwavunja moyo.
Walifahamisha
kupigwa kwao na mshangao na butwaa pale Vijana wa eneo hilo walipozuiwa
na Mtu huyo liyejitambulisha kulimiliki eneo hilo kutofanya shughuli
yoyote ya Michezo na Burdani katika Vipindi vya Siku Kuu za Iddi.
Akijibu
hoja na kutoa ufafanuzi wa Kilio cha Wananchi hao wa Shehia ya Mtofaani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwaahidi
kwamba atamuagiza Waziri anayehusika na masuala ya Ardhi pamoja na
Maofisa wake kwa kushirikiana na Uongozi wa Kikosi cha KMKM kufanya
uchunguzi wa kina kutambua uhalali halisi wa Mmiliki wa Eneo hilo.
Balozi
Seif ameamua kuchukuwa hatua hizo ili kupata Taarifa na Ripoti sahihi
itakayobainisha Mmiliki halali wa sehemu hiyo ili Serikali Kuu
itakapokuja chukuwa maamuzi isije ikaonea upande wowote.
Eneo
hilo la ardhi zamani likitumiwa kwa shughuli za ufyatuaji Matofali
lililojengwa ukuta wa matofali kati kati yake likiwa mashariki mwa
Msikiti Mkuu wa Ijumaa uliopo Mtofaani makutano ya Bara bara za
Masingini na Hawaii linakadiriwa kuwa na ukubwa wa eka Nne.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/11/2016.
COMMENTS