Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria ametembelea ubalozi wa Tanzania Brusels, Ubeligiji Septemba 29, 2017. P...
Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria ametembelea ubalozi wa Tanzania Brusels, Ubeligiji Septemba 29, 2017. Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji Mheshimiwa Joseph Edward Sokoine.
Prof. Kabudi yuko Mjini Brussels, Ubeligiji akiambatana na Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi. Wakati akiwa Brussels, Prof. Kabudi ameshiriki mazungumzo baina ya Rais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi baina ya Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Prof. Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja Bw. Geoffrey Kabakaki, Mwambata Maalum (Minister Plenipotentiary) wakati alipotembea makazi ya Balozi.

Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji

Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji

Picha ya pamoja
COMMENTS