WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akisisitiza jambo kwa wataalamu alipotembelea mradi wa maji Iyula halmashauri ya Mbozi, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya maji Mkoa wa Songwe Mhandisi Tanu Deule.

HomeJamii

WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe ametahadharisha kuwafukuza kazi na kuwashitaki wahandisi wa serikali wanaokosa uza...

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA MZITO MKOA WA ARUSHA
IBADA YA KUAGA WANAFUNZI WALIOFARIKI KATKA AJALI; UWANJA WAJAA POMONI
KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe ametahadharisha kuwafukuza kazi na kuwashitaki wahandisi wa serikali wanaokosa uzalendo na kuhujumu miradi ya maji katika hatua ya usanifu na usimamizi kwa kupitisha vifaa vilivyo chini ya viwango.
Mhandisi Kamwelwe ametoa tahadhari hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa miradi mitatu ya maji ya Iyula na Itaka katika halmashauri ya Mbozi, mradi wa Umwagiliaji Naming’ongo katika halmashauri ya Momba na mradi wa Maji Tunduma katika halmasahuri ya Tunduma.
“Miradi mingi inakamilika na kuzinduliwa na viongozi wakubwa wa kitaifa lakini mabomba yanaanza kupasuka muda mfupi tu baada ya wananchi kuanza kupata maji kwakuwa hayana viwango, wahandisi badilikeni na hili likitokea hauna ajira na kushitakiwa juu”, amesisitiza Kamwelwe.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi ya maji hakutakuwa na tija endapo shughuli za utafiti wa vyanzo vingine imara vya maji hazitafanyika pamoja na kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa ajili ya uendelevu wa miradi hiyo kwa muda mrefu.
“Hatutaki kusikia mradi unatoa maji kwa muda mfupi kisha maji yanaisha kwenye vyanzo, hivyo naagiza taasisi ya bonde la ziwa Rukwa washirikiane na taasisi nyingine pamoja na ofisi za wakuu wa wilaya kutafuta vyanzo vingine vya maji pamoja na ulinzi wa vyanzo vilivyopo”, amebainisha Mhandisi Kamwelwe.
Kwa Upande wao wananchi wameiomba serikali kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji katika hatua zote za ujenzi wa miradi tangu hatua ya usanifu ili kujenga uelewa juu ya miradi hiyo na kuondoa migogoro.
Ujenzi wa miradi ya maji ya Iyula, Itaka na Tunduma inatarajiwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi takribani laki moja ambao watakuwa wanapata maji kwa umbali usiozidi mita 400 sawa na mwongozo wa sera ya maji ya mwaka 2002.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akikagua chanzo cha maji Itaka katika halmashauri ya Mbozi pamoja na wataalamu wengine kutoka ngazi ya mkoa na wilaya.



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI
WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipAY17qKSKAglIZwly49Ws4yjvUI7-DjvblVIUEBfqmoS7070U5yZczAJulCwjMv5pNxRgmDMpmZHkess2yESE6PZgh11oqhwuSEfQCpbSfn5ouqDoWfJctVcnoATTV8SPq4gKpUghXpA/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipAY17qKSKAglIZwly49Ws4yjvUI7-DjvblVIUEBfqmoS7070U5yZczAJulCwjMv5pNxRgmDMpmZHkess2yESE6PZgh11oqhwuSEfQCpbSfn5ouqDoWfJctVcnoATTV8SPq4gKpUghXpA/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-wa-maji-kamwelwe-atahadharisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-wa-maji-kamwelwe-atahadharisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy