KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA
HomeJamii

KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA

 Mmoja wa viongozi wa vijana wa Chama cha  Tanzania Girl Guides  (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa (kulia), akilakiwa na Katibu wa Taifa wa TG...

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KUSOMESHA WAUGUZI NA WAKUNGA
ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA
WANAWAKE BARANI AFRIKA WAKUTANA TANZANIA KUJADILI AMANI YA BARA LA AFRIKA
 Mmoja wa viongozi wa vijana wa Chama cha  Tanzania Girl Guides  (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa (kulia), akilakiwa na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa wa Kimataifa wa  Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA, MATUKIO BLOG)


Na Richard Mwaikenda 

KIONGOZI wa Vijana wa Chama cha  Tanzania Girl Guides  (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa amefanya kazi kubwa ya kuwashawishi Wananchi wa Mexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania badala Kenya.


Dk. Mutasingwa ambaye alikuwa nchini Mexico kwa mafunzo ya miezi minne ya kubadilishana uzoefu katika nyanja za utamaduni na  uongozi alitumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya Tanzania.


Akizungumza  mara baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alisema kuwa moja ya mambo yaliyompa wakati mgumu ni kuwabadilisha wamexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya kama wanavyofahamu wao.


Alisema Wamexico wengi kwanza wanajua Afrika ni nchi, jambo ambalo pia ilibidi awaeleze kuwa  siyo nchi bali ni bara kama yalivyo mabara mengine duniani na katika bara hilo kuna nchi nyingi na mojawapo ni Tanzania anayotokea yeye.


Alisema akiwa huko licha ya kuwafundisha kiswahili pia alitangaza vivutio vingi  vya utalii vilivyopo nchini, ambapo aliwatajia wadudu, ndege za kila aina na  wanyama mbalimbali waliomo kwenye hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na nyinginezo.


Pia aliwafundisha kuhusu utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili, upikaji wa vyakula vya kitanzania kama vile ndizi na pilau, mambo ambayo walifurahishwa nayo.


Dk. Mutasingwa alisema kuwa ambaye katika ziara hiyo ya mafunzo alikuwa na vijana wenzie wa Girl Guids kutoka Venezuela,  Canada, Uingereza  na Argentina alipata wasaa wa kujifunza utamaduni wa mexico na kutoka nchi hizo zingine.


Alisema kuwa alijifunza mambo mengi ikiwemo ujasiri wa kufanya kazi bila woga, siasa za mataifa mbalimbali,  mambo ambayo ameahidi kuwafundisha vijana wenzie wa TGGA hapa nchini.


Dk. Mutasingwa aliwasili nchini jana, ambapo kwenye Uwanja wa Ndege wa JNIA, alilakiwa na Katibu wa Kitaifa wa TGGA, Grace Shaba pamoja na wanachama wenzie Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi.




 Dk. Mutasingwa akiwa na Katibu wa TTA Taifa, Grace Shaba (kushoto), Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi baada ya kulakiwa akitokea Mexico

Dk. Mutasingwa akifurahia jambo na  Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi.

 Dk Mutasingwa akikumbatiana kwa furaha na Maryrehema Kijazi

 Ni furaha iliyoje kukutana

  Dk. Mutasingwa akifurahi wakati akilakiwa na Elieshupendo Michael

Grace Shaba na Dk. Mutasingwa wakiwa na furaha
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA
KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMLI6gnocJ7lPaYn9NQDbhx6bFvUoLZsGXmirhjTw71osihr4mVpaXR-KOo_Nl-uPXJ7xcrbmWvrNxm0NFIuwFiu5h5CB1dpJ-PcA3OuuP5ocGh52UMvS20Gs8FeOjHujsQYtM4r6OLGs/s640/01.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMLI6gnocJ7lPaYn9NQDbhx6bFvUoLZsGXmirhjTw71osihr4mVpaXR-KOo_Nl-uPXJ7xcrbmWvrNxm0NFIuwFiu5h5CB1dpJ-PcA3OuuP5ocGh52UMvS20Gs8FeOjHujsQYtM4r6OLGs/s72-c/01.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/kijana-girl-guides-apambana-mexico-kuwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/kijana-girl-guides-apambana-mexico-kuwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy