FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI
HomeJamii

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini ...

KAMPUNI YA BIMA YA MGen INSURANCE YATOA MSAADA WA MASHINE ZA KIPIMA KIWANGO CHA HEWA NA MAPIGO YA MOYO KWA WATOTO WACHANGA
TSN,TBC ZA TWAA TUZO ZA DSE 2017 PIA ZIPO NMB, TBL NA STANDARD CHARTERED BANK
BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 29.09.2017





Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati akifungua  mkutano wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika chaguzi zijazo hapa nchini.


Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya serikali za mitaa na wa serikali kuu
wa mwaka 2020.



Hayo yamesemwa
mapema leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil
Society Bw. Francis Kiwanga alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye
lengo la kujadili hali ilivyo kabla ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani.


Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala mapema leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society.

Katika Mkutano
uliowakutanisha wadau kutoka Asasi mbalimbali za Kiraia, Taasisi za elimu ya
juu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya dini mashirika yanayoshughulikia amani
nchini  kujadili nafasi na wajibu wao
kama azaki kuelekea chaguzi zijazo hapa nchini.
Bwana Kiwanga
amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kupiga kura umekuwa ni mdogo sana
kwani 2010 wamepiga asilimia 43 peke yake na kwa mwaka 2015 ni asilimia 67 ya
wananchi wote wenye sifa za kupiga kura.


Baadhi ya washiriki kutoka asasi mbalimbali za kiraia wakifuatilia kwa umakini mkutano.

Ameeleza kuwa
 hii inatokana na wananchi kutokuwa na
imani na viongozi wanaochaguliwa kwani wanaamini hata usipopiga kura basi
mgombea wa chama fulani atapita kwa njia yeyote ile, hivyo taasisi zinazohusika
ikiwemo wizara ya tamisemi na NEC pamoja na ZEC kuboresha utendaji wao wa kazi
ili kurejesha imani hiyo kwa wananchi.



Amesema  kuwa asasi za kiraia zina jukumu kubwa la
kushirika katika mchakato kabla, kipindi chenyewe cha uchaguzi na baada ya
uchaguzi kwa kuwapa hamasa wananchi lakini pia kuomba nafasi za uangalizi
katika kipindi hicho.


Wageni waalikwa wakifuatilia mkutano kwa umakini.

Amesistiza
uhalali wa kuwapata viongozi ambao ni matwakwa ya wananchi kwani hii inaweza
kuleta kitu kizuri kwa kuwa atakuwa kapewa Baraka zote na wananchi na pia
watashirikiana nae kwa hali na mali kwa kuwa wanajua ndio chaguo lao sahihi.
Kwa upande
wake Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation amesisitiza uwepo wa
amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kwani amani ndio msingi
wa mambo yote.


Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uchaguzi ulioandaliwa na shirika la Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo jijini Dar es salaam.

Amesema  kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa
hivyo inapotokea watu wanamchagua mgombea Fulani alafu matokeo yanabadilishwa
na kupewa mtu mwingine hii sio sawa na inaweza kutowesha amani ya nchi

Lakini pia
hali ya mtu anatumia muda mwingi kwenye foleni ya kujiandikisha na mwisho wa
siku anaenda kupiga kura anaambiwa jina lako halipo kwenye daftari hali hii
inasababisha watu wengi kuacha kujiandikisha kupiga kura na kupoteza haki yao
ya msingi.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI
FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgR-qSOY08z220dhVKbwCNk5TctNCkLHatffJVIbn9h-Lyv7jDQua7tlKZe2fYGYO7LAYc7r5WdJP6HTp9QqOsN_02zvB_E-jHsuVez9X6HNu9nDMc0tSh9XNKv6xsHb9LKC2ETK4JMmw/s640/IMG_1792.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgR-qSOY08z220dhVKbwCNk5TctNCkLHatffJVIbn9h-Lyv7jDQua7tlKZe2fYGYO7LAYc7r5WdJP6HTp9QqOsN_02zvB_E-jHsuVez9X6HNu9nDMc0tSh9XNKv6xsHb9LKC2ETK4JMmw/s72-c/IMG_1792.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/foundation-for-civil-society-watoa-somo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/foundation-for-civil-society-watoa-somo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy