WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa baadhi ya viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea katika Ofisi yake Bungeni Dodoma Aprili 12, 2018.

HomeJamii

WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.

Na MWANDISHI WETU Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mha...

YUSUF MANJI AUNGANA NA FAMILIA YAKE, NI BAADA YA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KUFUTWA
UINGIZAJI WA MIFUGO KWENYE PORI LA AKIBA LA MKUNGUNERO UMEADHIRI UHIFADHI
JHPIEGO LAUNCHES PROJECT TO SCALE UP FAMILY PLANNING SOLUTION IN URBAN CITIES


Na MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendela kuliombea Taifa ili kudumisha Amani na Utulivu uliopo.
Ametoa pongezi hizo hii leo alipokutana na Uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza Serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.
“Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo.”Alisema Waziri Mhagama
Aliongezea kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wetu wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kufikia azma yake ya “Tanzania ya Viwanda”.
“Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu Uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na Viongozi wote kwa ujumla wao ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo.”Alisisitiza Waziri Mhagama
Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika Huduma za kijamii hususan kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na Shule, Vyuo na Zahanati zinazohudumia Wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.
“Ni vyema sasa mkawa na mipango endelevu ya kuboresha Taasisi zenu ikiwemo Chuo cha Mount Meru na shule zenu ili kuendelea kutoa huduma za kielimu, afya ili kuwa na Watanzania wenye uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.”Alisisitiza Waziri.
Aidha kwa upande wake  Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.
“Binafsi ninaipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa juhudi zake pamoja na uongozi wote na tunaahidi kuendelea kuwaweka mikononi mwa Mungu ili kuwa na nchi yenye Amani, Upendo, Mshikamano na Utulivu.”Alisisitiza Askofu Manase.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kanisa la Baptist nchini.


Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza masuala yao na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada za kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipata maelekezo ya hati ya pongezi (ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli) kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwashukuru viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.
WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0MK7RzDKBrPwn9bOubPnN7P1OVEEgRXjD22QzuwDc6QeSKpWIiVjlfd-2abk1bksbb1CA03V41D9CrXMF0jYB4BIa41q8hrpbCmm-uHsEhBQa4SUt87VG8wXaJmzPsnmLSplD8iDyK9k/s640/P1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0MK7RzDKBrPwn9bOubPnN7P1OVEEgRXjD22QzuwDc6QeSKpWIiVjlfd-2abk1bksbb1CA03V41D9CrXMF0jYB4BIa41q8hrpbCmm-uHsEhBQa4SUt87VG8wXaJmzPsnmLSplD8iDyK9k/s72-c/P1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-mhagama-aupongeza-uongozi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-mhagama-aupongeza-uongozi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy